HER MOTHER'S DAUGHTER (Episode ya 67) JULIO APIGWA RISASI, HUKU MARGAUX NA CELYN WASAMEHEANA.
![]() |
| Beatrice (kulia) Julio, Yolanda, Lucas na Margaux mwisho. |
Celyn, Magaux, Yolanda na familia yote ya Theresa wakiwa katika sherehe ndogo nyumbani kwao wakisherehekea kutoka jela kwa mzee Zacharis, ambapo pia Julio alikuwa ni mmoja kati ya wanafamilia hao. Theresa alitoka nje ya nyumba na kumkuta Diego dereva wa Yolanda akiwa nje ya geti, lakini Theresa aliamua kumkaribisha ndani na kumpatia chakula.
Julio aliamua kuaga na kuondoka kuelekea alikokuwa amepaki gari lake, ambapo pia Diego alikuwa kaishatangulia nje. Kumbe kunaunyama ulikuwa ukitaka kufanyika pale katika nyumba ya Theresa. Alitokea mtu mmoja akiwa amevalia kofia ambaye pia ni baba yake Diego (Joshua) Diego alipomuona akiwa ameshikilia bastola alishtuka na kumuuliza kuwa anatafuta nini? Alimjibu kuwa yuko kazini na kumfuata nyuma Julio.
Alipomfikia Julio alimnyooshea bastola, huku Diego akiwa anawaangalia, ndipo Julio alipomdaka mkono wa jambazi na kuanza kuvutana, ghafla simu ya Julio ilijipiga yenyewe mfukoni na kwenda kwa Celyn. Celyn alishtuka na ghafla alisikia mlio wa risasi ndipo alipotoka nje na kumkuta baba yake akiwa amelala chini akiwa tayari amepigwa risasi.
Margaux na akina Theresa wote walitoka nje na kuungana na Celyn huku jambazi akiwa tayari amekwisha tokomea, huku akitumia gari jekundu alilochukua kwa Diego. Walifanikiwa kumkimbiza hospitali huku pia wakimpigia simu Beatrice mke wa Julio.
Beatrice japokuwa walikuwa na mgogoro na Julio lakini aliwasili hospitali haraka sana huku machozi yakimbubujika machoni. Diego alionekana kuwa ni mwenye wasiwasi kwani alishuhudia tukio zima lililofanywa na baba yake. Baadae polisi waliwasiri hospitali na kuzungumza na Celyn ambaye ndiye aliyemkuta baba yake kiwa chini baada ya kupigwa risasi tumboni.
Celyn aliwaambia polisi kuwa mtu aliyeshuhudia tukio ni Diego hivyo wamuulize, polisi walimfuata Diego na kupata maelezo japokuwa alikwepa na kusema hakumuona mharifu kwani angemuona angemkamata. Celyn kusikia hivyo aliwasisitiza polisi kumuhoji tena na polisi waliahidi watafanya hivyo.
Jambazi baada ya uharifu alitokomea na gari nyumbani kwa Diego, ile anafika na gari Ethan alikuwa jirani kabisa na nyumba ya ya Diego hivyo alihisi kitu na kwakuwa alikuwa anaelekea hapo kumpelekea pesa Diego, hivyo hakusita kufuatilia hadi mlangoni akapiga hodi. Yule jambazi alitoka nje na Ethan kuuona mkono wake mmoja ukiwa umejipaka damu. Ethan alimuulizia Diego na kuondoka.
Tayari Ethan amekwisha mshitukia baba yake Diego kuwa ni mtu mbaya, na huko hospitali Julio anapelekewa picha kadhaa na ili achague mtu aliyempiga risasi, kwa bahati nzuri alimtambua baba yake Diego. Picha hiyo ilipelekwa kwa wanafamilia wote wakashindwa kumtambua lakini Teresa tu ndiye aliye mtambua, ghafla Lucas alipata wasi wasi kwani yeye ndiye aliyemtuma yule jambazi kufanya mauwaji.
Kutokana na tukio la Julio kupigwa risasi Margaux na Celyn wakiwa wote wanabubujikwa na machozi wamejikuta wakikumbatina na kuzizika tofauti zao za sikunyingi huku Margaux akilia na kumuomba msamaha Celyn. Baada ya hapo walielekea katika chumba alikolazwa baba yao.
Wakiwa katika chumba hicho Celyn alitaka kuondoka kwenda kumuita nesi, lakini Julio alimzuia na kushika mikono yao wote na kusema kuwa "ninachowaomba nyote mabinti zangu ni mpatane" Margaux alitambasamu na kusema "Baba mimi na Celyn tumekwisha kuwa marafiki tena". Baada ya hapo hali ya Julio ilibadilika ghafla na kupoteza fahamu.
DONDOO ZIJAZO:
Je Julio ndio amefariki baada ya binti zake kupatana? Na je Lucas atachukua maamuzi gani baada ya Theresa kumtambua jambazi wake? na Je Ethan tayari amekwisha mshitukia baba yake Diego je atasaidia upelezi? Hatahivyo Jambazi ameingia ndani ya gari la Diego tayari kwa kutoroka, lakini Ethan anawafatilia kwa nyuma, je nini kitatokea? Fuatilia dondoo zijazo hapa hapa Asili Yetu TZ.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA