HER MOTHER'S DAUGHTER (Episode ya 61) NDOA YA BEATRICE NA JULIO YASAMBARATIKA.
![]() |
| Beatrice |
![]() |
| Julio |
Celyn pia ameonekana kuwa karibu na babu yake hasa pale alipogundua kuwa babu huyo hali yake sii nzuri kiafya. Lakini kwa upande wa Beatrice yeye baada ya kuona mambo ya familia yake hayaendi vizuri, basi aliamua kuomba msaada kwa Lucas yani baba yake ili amshitaki mahakamani Zacharis kwa kuwaficha siri za mabinti zao kwa muda mrefu.
Beatrice na baba yake wanapanga njama za kumfunga tena jela Zacharis, lakini kabla ya kufanya hivyo, Lucas anamjengea mazingira magumu mkewe Yolanda ambaye walikuwa wameachana kumtaka arudi nyumbani, la sivyo anaweza kumfanyia Zacharis kitu kibaya. Yolanda kwa mapenzi aliyonayo bado kwa mume wake wa zamani Zacharis, basi anaamua kukubali masharti ya Lucas na kurejea nyumbani, japokuwa Theresa na baba yake wameshaanza kuhisi kitu kibaya katika hili jambo.
Celyn akiwa ofisini, mara anaingia katika ofisi ya Liam na kumkuta Margaux akimshika shika Liam, mara Liam anashtuka sana kumuona Celyn na kunyanyuka haraka. Lakini Celyn anaonekana kushikwa na wivu japo hawezi kusema wazi, aliondoka kwa hasira.
Margaux tayari amekwisha rejea mjengoni na safari hii amepanga kupokonya madaraka yote ya pacha wake Celyn. Lakini pia kule nyumbani kwao kizaa zaa kinatokea baada ya Beatrice kumwambia Julio kuwa anataka kumshitaki Zacharis mahakamani. Julio anashangazwa sana na maamuzi ya Beatrice na kumwambia kuwa "tokea nikuoe sijawahi kupata amani ndani ya moyo wangu, kwani kila mara ni ugomvi tu, hupaswi kuishitaki familia ya Zacharis kwani hata wewe unamakosa, usitake kujisafisha kwa kuwalaumu wenzio, sasa mimi nimechoka na leo imevunjiaka" Julio alitamka maneno haya kwa huzuni na kumuacha Beatrice mdomo wazi. Julio alichukuwa mabegi na kuchapa mwendo kusiko julikana.
Margaux baada ya kutoka kazini alimuomba Liam amsindikize anapoishi, Liam alimsindikiza mpaka mlangoni na kumuacha pale na yeye kuondoka. Lakini Margaux alipigwa na butwaa pale alipoingia ndani na kukuta kila kitu kikiwa hovyo hovyo, kwani alihisi kunajambazi ndani, hivyo alimpigia simu haraka Liam kuwa kunajambazi ndani.
Margaux aliamua kushika chupa mkononi na kuanza kunyata ndani akitafuta mbaya wake alipo, mara alitokea mtu akiwa ameficha uso wake kwa boshori nyeusi, na kumvaa Margaux, walipambana kidogo na yule Jambazi kuamua kukimbia. Lakini wakati anatoka walipishana mlangoni na Liam, ndipo Liam alipokwisha kuhakikisha kuwa Margaux yuko salama, ndipo alipomgeukia kumfukuza jambazi.
Jambazi walipambana na Liam, lakini kwa bahati mbaya jambazi alimzidi nguvu na kutokomea. Liam aliamua kurudi kwa Margaux ambapo pia Margaux alijaribu kumpigia baba yake na mama yake simu bila mafanikio, ndipo Liam akatoa wazo kuwa kwanini usimpigie mama Theresa? Walimpigia simu kwani alikuwa tayari nyumbani na Celyn.
Theresa alikuja haraka na kumkumbatia Margaux, wote walimwaga machozi ya kutosha na kuamua kwenda wote nyumbani. Celyn na babu yake walikuwa wakiwangoja nyumbani. Margaux aliandaliwa chumba chake cha kulala na kulala. Siku iliyofuta wote wakiwa mezani mama yao alionekana kuwa na furaha isiyo na kifani kwani alifurahi kuwaona watoto wake wote wawili wakiwa pamoja nae.
Ghafla Julio aliwasili hapo kwa Theresa baada ya kuwa amekuta ujumbe wa simu ya Magaux, walizungumza wote na Julio kuondoka , lakini baada ya muda mfupi Beatrice nae aliwasili pale na kumtaka Margaux aondoke nae, lakini Margaux alikataa kata kata na kuondoka na kuamua kubaki kwa Beatrice.
DONDOO ZIJAZO:
Diego ndiye jambazi aliyevamia nyumba ya Margaux na kuharibu vitu, ameanza kulipiza kisasi alichosema? Je anatatizo gani na Margaux? na vip kuhusu ndoa ya Julio na Beatrice itarejea kama kawaida? Je Margaux ataendelea kuishi kwao Celyn au ataondoka? Fuatilia hapa hapa ASILI YETU TZ.


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA