HER MOTHER'S DAUGHTER (Episode ya 57 & 58) KIZAA ZAA CHAIBUKA BAADA YA MARGAUX KUJUA KUWA THERESA NI MAMA YAKE.
![]() |
| Margaux |
Margaux akiwa katika sherehe ya kuzaliwa kwa baba yake Julio Marasigan, mara anapigiwa simu na Ethan kuwa tayari amekwisha mpata yule mkunga. Margaux aliondoka kwa haraka sana huku akimpigia simu Beatrice mama yake wa kuasili na kumwambia anakoenda. Beatrice aliingiwa na wasi wasi sana na kujaribu kumzuia Margaux asiende peke yake, lakini Margaux alipuuza.
Kule Ethan na Margaux alimbembeleza yule mkunga mpaka akawambia kuwa, Teresa alijifungua watoto mapacha, wakati huo akiwa na binamu yake Oscar, na mtoto mmoja alifichwa na kupelekwa kwa Beatrice, hivyo huyo mtoto ni yeye "Margaux".
Baada ya Margaux kujua ukweli huo, aliondoka kwa ghadhabu na kuwafata mama na baba yake yani Julio Marasigan na Beatrice huko katika Sherehe. Huko kwa Teresa alikuweko Zacharis ambaye hakuhudhulia sherehe ya kuzaliwa kwa Julio, bali walipanga mbinu na mke wake wa zamani Yolanda Cruz ambaye ni mke wa Lucas Elzalde, jinsi Zacharias Apolinario atakavyoweza kutoboa siri ya kuwa Theresa alijifungua watoto mapacha ambao ni "Margaux na Celyn".
Margaux anawasili akiwa ni mwenye jazba na kumuita Beatrice kwa sauti, Beatrice anajitokeza na Julio pia, Margaux anawaeleza kuwa wakati akiwa mdogo, Beatrice alimchukua kutoka kwa Theresa, akipewa na Oscar.
Wakati jambo maelezo hayo yakimtoka Margaux ndugu wote walikusanyika, lakini Lucas babu yake Margaux alijitokeza na walinzi wake na kumnasa kibao Oscar, huku walinzi wakimtia nguvuni. Beatrice na Theresa wote walijawa na asira hiyo walimtandika Oscar vibao vya kutosha, lakini Julio alijaribu kuwazuia.
Ndipo Zacharis na Yolanda walipowasili, na mzee Zacharis kuamua kumsaidia mzigo Oscar na kusema, makosa yote yaliyofanywa anapaswa kulaumiwa yeye. Baada ya hapo nyumbani Theresa anazira kukaa na ndugu zake, hivyo anapangishiwa hoteli na mwanae Celyn.
Julio naye anamkasilikia mkewe Beatrice kwa kumficha siri kwa miaka 20 sasa, hivyo tayari tatizo lingine limeibuka ndani ya mahusiano ya Julio Marasigan na Beatrice. Theresa naye anafunga safari hadi kwa Beatrice ili kuonana na mwanae mpya Margaux, lakini anarudishwa na Beatrice mlangoni.
Dondoo zijazo: Je kuna nini kati ya Diego Madina na familia ya Theresa? , Margaux anaonekana wakikumbatiana na mama yake mpya yani Theresa, je Margaux ameamua kuja kuishi kwa Teresa? Je penzi la Ethern na Margaux ndo limerejea upya kwa mtindo huo na je Lucas atachukua uamuzi gani baada ya kuwaona Yolanda na Zacharias wakitokomea garini? Julio na mkewe Beatrice je?
Fuatilia dondoo zijazo za kusisimua hapa hapa ASILI YETU TANZANIA. Pia usikose ku LIKE ukurasa wetu Face book. Bofya "Asili YETU Tanzania".

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA