UTAMU WA TAMTHILIA YA "HER MOTHER'S DAUGHTER" SASA NJE NJE (Episode ya 55)..
| Celyn |
Muendelezo wa msichana Margaux wa kuwatafuta wazazi wake halisi, unazidi kuchukua sura mpya hasa pale baba yake yani Julio anapoonekana kumpa moyo katika swala la kuwatafuta wazazi wake. Lakini pia kutokana kuwa Beatrice anampenda mwanae Margaux, basi nae ameungana nae katika kuwatafuta.
Beatrice anamfuata Oscar na kumuomba amuambie jina nesi aliye wapatia mtoto yapata miaka 20, ambaye sasa ni Margaux, lakini Oscar anasema hamkumbuki kwasababu ni siku nyingi. Beautrice inabidi atumie ukali kidogo, ndipo japo alikubali kumuelekeza eneo huenda akawa yupo.
Beatrice na Margaux wanafunga safari hadi eneo hilo na kuanza kumsaka bila mafanikio, huku wakiwa wamemuweka mtu maalum wa kufanya pia uchunguzi kuhusiana na wazazi halisi wa Margaux. Lakini pia kunamtu yuko jela huenda anahusika na kati ya siri nzito zilizo jificha.
Kati ya watu waliohusika kumuiba Margaux wakati akiwa mdogo na kumpatia Beatrice, ni Zacharias na Oscar. Kwani sasa waingiwa na wasi wasi mkubwa baada ya kusikia Beatrice na Margaux wanataka kujua ukweli, wapanga kusema ukweli lakini roho bado zinasita.
Kwa upande wa msichana Celyn, mambo yanazidi kumnyookea, baada ya kuteuliwa tena kukaimu nafasi ya Margaux wakati akiwa likizo. Hata muonekano wa Celyn siku hizi unazidi kuvutia macho ya mfanyakazi mwenzake, yani Liam.
Baada ya masaa ya kazi kuisha, msichana mrembo Celyn aliingia garini tayari kuelekea nyumbani kwao, lakini alipoingia katika gari hilo, yeye alifahamu kuwa aliyekuwa akiendesha ni dereva wake wa siku zote, lakini kumbe alikuwa ni Liam.
Liam alimtaka waongee kuhusu sula la mahusiano yao, kwani Celyn amekuwa akimkwepa siku hadi siku bila mafanikio. Lakini Celyn alipojua kuwa hakuwa dereva wake, alikuwa ni Liam basi akamsihi ampeleke nyumbani. Lakini Liam alichepukia katika njia tofauti na yanyumbani na kutokomea.
Celyn alinyanyua simu na kutaka kupiga polisi, lakini Liam aliinyakua na kuitupa nje ya gari. Walipofika katika eneo la ufukwe Liamu alipaki gari pembeni na kuanza mazungumzo na Celyn ambaye bado alikuwa hataki kabisa kumsamehe Liam ili wawe wapenzi.
Celyn alipanda katika ukingo wa bahari na kumtaka Liam achague moja, kumpeleka nyumbani au ajitupe baharini. Liam alipigwa na butwaa na kumuuliza "kwahiyo umeona kuliko kunikubalia tuwe wapenzi ni bora ujitupe baharini?" Celyn akajibu "Ndiyo". Basi Liam akamwambia kwa hasira okay twende nikupeleke.
Katika dondoo zijazo, Ethan baada ya kupata kazi katika kampuni moja hivi, kumbe yaja kubainika kuwa ni ya mbaya wake "Lucas". Na pia Lucas anawaagiza wafanyakazi wake wafanye kila njia wamfukuzishe kazi Ethern. Je nini kitatokea endapo watamfukuza kazi, je atawafungulia mashtaka? Je Celyn atamkubalia Liam?
Margaux anaonekana akiwa na Ethan na Etahan anasikika akimwambia Margaux kuwa "nitakusaidia kuwatafuta wazazi wako". Fuatilia dondoo zijazo hapa hapa Asili Yetu Tanzania. BOFYA HAPA KULIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA