Header Ads

Breaking News
recent

TAMTHILIA YA "HER MOTHER'S DAUGHTER" (Episode ya 52) MSICHANA MARGAUX AGEUZIWA KIBAO.

 Katika episode iliyopita msichana Margaux alionekana kutamba katika uzalishaji wa viatu vya bei ya juu na katika kampuni yao ya kutengeneza viatu inayoitwa "Memorata", kitu kilichomtia Celyn wasi wasi wa kunyang'anywa kitengo chake na kujaziwa kwa Margaux.

Lakini Mungu si Athuman sasa mambo yamgeukia baada ya kitengo cha Celyn kuongezekia kimauzo na kukijengea kitengo cha Margaux mazingira ya  matumizi makubwa ya kutengeneza viatu vya bei ya juu.

Margaux akiwa anapita alisikia bodi ya Memorata ikiwa inazungumzia uzarishaji wa kampuni hiyo, huenda Margaux alijipa moyo kuwa walikuwa wakizungumzia utendajiwake kazi kuwa na manufaa makubwa. Lakini mambo yalikuwa kinyume baada ya yeye kuitwa na kuambiwa atoe tathmini yake katika mradi wake wa viatu vya bei ya juu.

Margaux alijieleza kwa akijiamini, kuwa "mwaka huu tumeanguka kimauzo, lakini tutafanya bidii mwaka ujao tuuze viatu vyetu nchi mbali mbali na hivyo ninauhakika tutafanya vizuri" lakini mjumbe mmoja alimkatika na kumuambia wao hawana malighafi za kutengeneza viatu hivyo vya gharama, kwani vinahitaji pesa nyingi.

Kule ofisini Liam alimletea Celyn habari njema kuwa, idara yao imeongeza mauzo mara dufu, hivyo Liam alitaka kumtoa Celyn faragha wakasherehekee wawili ili pia apate mwanya wa kukumbushia mahusiano yao ya hapo awali. Lakini Celyn akiwa na furaha alinyanyua simu na kuwapigia wafanyakazi wote na kujumuika nao kwa chakula.

Margaux tayari amekwisha umbuka, anaonekana ni mwenye hasira na baada ya mradi wake kukataliwa. Pia wakati Margaux akiwa nje ya ofisi, Ethan alimtokea na kumuomba waongee, alikini Margaux alikataa na punde babu yake Margaux aliwasili na kumgombeza sana Ethan huku Margaux akimsingizia kuwa alikuwa anamtafuta Celyn.

Teresa mama yake Celyn aamua kurudi shule kumalizia masomo yake, hivyo watasoma na Ethan kwani na yeye ameamua kumalizia masomo yake. Je Celyn atafurahi mama yake kusoma na Ethan? Beatrice nae amuandikisha Celyn kama mrithi katika familia yao, je Margaux akifahamu atachukuwa uamuzi gani?

Fuatilia dondoo nyingine hapa hapa Asili Yetu Tanzania Blog. Karibu sana!

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.