Header Ads

Breaking News
recent

PICHA: OPRAH WINFREY AFUNGUA MRADI WA MAJANI YA CHAI YENYE JINA LA KISWAHILI "OPRAH CHAI TEA".

Mwanamke maarufu na mtangazaji wa show za Luninga Marekani, ambaye pia hivi majuzi aliitembelea Tanzania katika mbuga za wanyama, mwanamama huyo maarufu kama Oprah Winfrey ameanzisha mradi wa majani ya chai aliyoyapa jina la "Oprah Chai Tea".

Hii ni aina mojawapo ya majani hayo ambayo yatakuwa na radha tofauti tofauti, huku mauzo ya majani hayo yatasaidia shule yake ya wasichana ya "Oprah Winfrey Leadership Academy" iliyoko Afrika ya Kusini

Majani hayo pia yanategemewa sokoni mwezi April 29 mwaka huu, ambapo yataanza kuuzwa Nchini Marekani na Canada.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.