Header Ads

Breaking News
recent

TAMTHILIA YA HER MOTHER'S DAUGHTER (Episode ya 50 & 51) WIVU WAZIDI KUTAWALA.

Baada ya Margaux kulejea tena Nyumbani, mambo kwa Celyn yaanza kwenda tofauti kutokana kuwa wote wanafanya kazi sehemu moja, katika kampuni ya baba yao, inayoitwa "Memorata".

Wasichana hao kutokana kuwa na ushindani wa hali ya juu katika kubuni njia mbali mbali za kuzalisha viatu, wanajikuta wakipewa vitengo tofauti, ambapo Margaux yeye anapenda kuzalisha viatu vya gharana, huku mwenzake Celyn akielekeza ubunifu wake katika kutengeneza viatu vya bei ya chini vitakavyowafaa watu wote.

Katika mradi mpya wa Celyn wa kutengeneza viatu vya bei ya chini, unaingia katika wakati mgumu baada ya Margaux kumuomba baba yake avunje mradi wa Celyn na kuongezea nguvu katika mradi wake.

Ethan bado hajakata tamaa kwa Margaux, anamfuata mida ya jioni na kumuomba wazungumze, lakini Margaux anakataa na kudai kuwa hana muda wa kuzungumza na yeye. Wakati Margaux akiondoka, mara anadondosha bahasha, Ethan anaiokota, huenda ikawa ni tiketi ya kuhudhulia tamasha la uzinduzi wa bidhaa mpya za Memorata.

Ethan anaiokota na kumuita Margaux lakini hakugeuka, alindelea na safari yake. Huko nyumbani mida ya asubuhi ambapo ilikuwa jioni yake ndio uzinduzi, Beatrice alienda chumbani kwa Margaux na na kuanza kumchagulia nguo za kuvaa, lakini Margaux alimuuliza mama yake kwanini asingeenda kumchagulia Celyn?

Wakati huo Celyn alikuwa mlangoni lakini hawakumuona, Beatrice akajibu "Siunamjua Celyn alivyo?" huenda Celyn hakupenda kauli hiyo. Lakini pia Beatrice alimfuata Celyn na kumtaka akubali kusimamisha idara yake ya viatu vya bei rahisi ili wampe Margaux mtaji huo.

Lakini Celyn alimjibu mama yake kuwa, yeye amekuwa mvumilivu kwa kila jamba, hata ambapo amekwisha kuwa mtoto wao? Beatrice alishtuka na kumuomba asifikilie hivyo. Lakini pia Julio baba yake na Celyn hakupenda kauli ya Beatrice hivyo alimsihi kutofanya hivyo tena, lakini Beatrice alijitetea kuwa yalikuwa ni maoni tu.

Kwa upaende wa Liam anazidi kufanya jitihada za kila aina ili arudishe upendo wake wa mwanzo kwa Celyn, lakini Celyn bado amekuwa mgumu kwa hilo. Siku ya uzinduzi umewadia lakini Celyn hauenda katika uzinduzi huo, bali elindwa kwao kwa mama yake Teresa na kumpa zawadi ya nyumba kubwa.

Je nini kitakachoendelea, endapo Julio na Beatrice wakigundua Celyn amewapangishia kwao nyumba mpya? Je ile karatasi aliyookota Ethan itakuwa na majambo gani? Fuatilia dondoo hizi hapa hapa Asili Yetu Tanzania.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.