Header Ads

Breaking News
recent

TAMTHILIA YA "HER MOTHER'S DAUGHTER" (Episode 21 & 22). PENZI LAINGIA DOSALI.

Margaux (kushoto) na Celine (kulia)

Baada ya Tamthilia ya kusisimua ya "Her Mother's Daughter" kupotea machoni kwa mashabiki, sasa yarudi kwa kishindo, ambapo penzi la Ethan na Margaux lazidi kutia shaka na kuingia katika dimbwi refu la misuko suko.

Bado mama yake Teresa anapata wakati mgumu wa kumtafuta binti yake Teresa, ambaye ni mama yake Celine, lakini pia Teresa na baba yake wanaingiwa na hamu ya kutaka kukutana nae. Katika upande wa Ethan  na Rio bado kunautata ambao kila mmojawapo anamtamani msichana wa mwenzake.

Lakini pia kwa upande wa Margaux na Celine mambo ni yale yale, wivu wa kichini chini unatanda kati yao baada ya mama yake Ethan kutoka hospitali na familia ya Rio kuamua kumfanyia sherehe. Hivyomama yake Rio anamuagiza Ethan amualike mpenzi wake ambaye wote walidhani kuwa ni Celine japokuwa ni Margaux.

Kwa kuendelea kuficha ukweli kuwa mpenzi wa Ethan ni Margaux, Ethan anaamua kumchukua Celine na kumtambulisha kwa mama yake, lakini kabla ya Celine kwenda, Margaux anampatia nguo nzuri na kumuweka sop sop ili asiaibike huko aaendako. Baada ya hapo Ethan alimfuata Celine na kuondoka nae.

Huku nyuma Margaux alibaki akiwa ni mtu mwenye mawazo, akifikilia kuwa nafasi hiyo ya utambulisho ulikuwa ni wake, lakini kutokana na familia yake pamoja na babu yake kutompenda Ethan, basi ilibidi ukweli wa penzi lake na Ethan uendelee kuwa siri.

Margaux aliamua kumuelezea bibi yake ukweli kuwa, wamekuwa katika penzi la kificho na Ethan mara kwa mara, huku wakimtumia Celine kujifanya ndiye mpenzi wa Ethan, kumbe laa! Ukweli aliopewa na bibi yake kiasi flani ulimfungua macho, kwani bibi yake alimuasa kuwa, njia aliyoitumia ya Celine kujifanya mpenzi wa Ethan sio sahihi, kwani kufanya hivyo ndivyo alivyozidi kuzidisha matatizo.

Mama yake Celine hapendi kabisa binti yake kujenga mahusiano na familia yao Margaux, kwani anajua kuwa baba yake Margaux, yuko katika uchunguzi wa kutaka kumjua binti yake waliyozaa na Beatrice (mama yake Celine).

Baba yake Margaux anamualika Celine katika chakula, faragha huko mgahawani, huko alimdadisi Celine mambo mengi, yaliyompelekea aendelee kuamini kuwa huenda Celine akawa binti yake. Siku ile Celine aliyoenda kujiaandaa kwao Margaux akitaka kuelekea katika sherehe ya mama yake Ethan, baba yake Margaux alifanikiwa kuchukua nywele za Celine zilizokuwa katika chanuo, na kuzipeleka katika vipimo vya Vina Saba (DNA).

Baada ya siku kadhaa kupita, bibi yake Margaux alimwambia Margaux awaalike marafiki zake katika sikukuu yake ya kuzaliwa, siku iliwadia, Margaux, Celine, Ethan na Rio walielekea katika sikukuu. Kama kawaida babu yake Margaux alimzingua Ethan, lakini bibi yake Margaux alimzuia na Ethan kuendelea kujivinjali.

Ghafla Ethan anamuacha Margaux na Rio mezani na kumuomba Celine waende wakacheze muziki, Celine kwa shingo upande anakubali, hivyo Ethan anamshika begani na kiunoni Celine na kuanza kucheza nae kama mpenzi wake. Wivu unamshika Margaux naye anamua kucheza na Rio.

Tayari Ethan anaonekana kuanza kuzama katika katika penzi jipya walilokuwa wakidanganya, lakini sasa laelekea kuwa kweli. Kwa upande wa Rio na Margaux nao hisia zinaanza kushabihiana, huku kila mmoja akionekana kumtaka mwenzake.

Je Ethan atazama katika penzi la Celine? Na je Margaux naye ataendelea kutaka penzi la Rio? Vipi kuhusu majibu ya vipimo vya Vina Saba (DNA) alivyochukua baba yake Margaux, sasa vyaonyesha kuwa Celine ni binti yake, je itakuwaje? Fuatilia dondoo za Thamthilia hii hapa Asili Yetu Tanzania.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.