MUENDELEZO WA TAMTHILIA YA "HER MOTHER'S DAUGHTER" (Episode ya 23) SIRI NZITO YAFICHUKA.
Utamu wa Tamthilia hii ndio kwanza umeanza, baada ya siri nzito za wapenzi, ndugu na jamaa kuanza kuwekwa wazi ambapo tayari Margaux ameshindwa kujizuia na kumuuliza rafiki yake Celine kuhusiana na hali ya msichana huyo kuonyesha kumtamani mpenzi wake Ethan.
Utafiti wa baba yake Margaux kuhusu vipimo vya Vina Saba alivyokuwa akivifanyia uchunguzi, sasa vya pamba moto, huku nyumbani kwao Celine nao wazidi kujawa na hofu kuhusiana na upelelezi wa baba yake Celine kuhusiana na familia hiyo.
Celine akiwa katika sherehe ya kuzaliwa kwa Yolanda (bibi yake na Margaux) anapigiwa simu na Zacharias yani babu yake ambaye alikuwa ni mume wa zamani wa Yolanda, kuwa ataenda kumchukuwa mara baada ya sherehe. Kwani nia ya mzee huyo alikuwa angalau amtie machoni mke wake Yolanda ambaye ni takribani miaka ishirini hajamuona baada ya kupokonywa na kutiwa jela.
Babu huyo aliamua kumfuata mjukuu wake Celine huko shereheni, kiukweli alisogea na kujibanza sehehemu wakati sherehe ikiendelea, mkononi alikuwa ameshikilia zawadi ambayo Yolanda alikuwa akiipenda kila mara siku yake ya kuzaliwa ilipowadia.
Zacharias alimpatia mtu zawadi ile aifikishe kwa Yolanda, lakini baada ya Yolanda kuifungua zawadi ile alipigwa na butwaa na kung'amua kuwa zawadi ile ilitokwa kwa mume wake wa zamani ya babu yake na Celine. Ghafla alinyanyuka na kuanza kumtafuta, lakini akafanikiwa kumuona kwa mbali na baada ya hapo mzee yule alitokomea.
Teresa kuambiwa kuwa baba yake ameenda katika sherehe hiyo, aliamua kumfuata kule ili kuwaondosha kule pamoja na Celine. Alipofika pale alimpigia simu Celine akaja, lakini kabla hawajaondoka, baba yake Margaux aliwasili hapo na Celine bila kujua alimtambulisha mama yake Teresa, kitu ambacho kilimfanya baba yake Margaux aamini kuwa Celine atakuwa binti yake.
Hofu tayari imekwisha tanda kati ya penzi la Margaux na Ethan, Margauxanaamua kuvunja ukimia na kumuuliza Celine kama amemzimia mpenzi wake Ethan, lakini Celine anajifanya kutokuwa na hisia yoyote na Ethan. Ghafla Ethan anampigia simu Celine aende kwao kwani mama yake alikuwa akilia na kumtaka mume wake atafutwe arejee. Celine alienda na kumyamazisha mama huyo kwa kumuimbia wimbo alioupenda.
Baada ya hapo wote walionekana kuwa na ishara ya kutakana mahusiano. Siku hiyo usiku Ethan aliamua kumpigia simu mpenzi wake Margauxna kumtaka wazungumze kuhusiana na uhusiano wao. Ethan alisema umefika muda sasa wa kila mmoja wetu kuvunja ukimia na kuweka mambo wazi, Margaux alikuwa akimsikiliza huku machozi yakimbubujiaka kama maji ya mtoni.
Kilichokuwa kikimliza Margaux sii kingine ni pale anapomuona Ethan akizidisha mapenzi zaidi kwa Celine. Baada ya Sherehe kumalizika Teresa na baba yake waliamua kufungasha mizigo yao na kutaka kurudi kijijini walikokuwa wakiishi mwanzoni, ili kumtorosha Celine asichukuliwe na familia yao Margaux.
Kabla hawajaondoka Celine aligoma kwenda mpaka wamwambie kuna nini wanachomficha, lakini pia baba yake Margaux anamfuata mama yake Celine na kumuonyesha majibu ya Vina Saba (DNA) kuwa Celine ni binti yake. Mama yule anahaha kusikia hivyo. Lakini hiyo haitoshi baada ya tukio hilo sehemu nyingine Teresa na baba yake wakiwa wamesimama, ghafla mama yake ana muita kwa nyuma... whaat! tayari pamoja na kujificha kwa muda mrefu sasa apatikana.
Mama yake Margaux baada ya kusikia kuwa Celine ni binti yao, anakasirika sana na kusema atahakikisha kuwa binti yake Margaux hatokuwa na uhusiano tena na Margaux. Je nini kitaendelea? Fuatilia hapa hapa Asili Yetu Tanzania.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA