TAMTHILIA YA "HER MOTHER'S DAUGHTER" (Episode ya 20) SASA NI UHONDO MTUPU.
Wapenzi wafuatiliaji wa Tamthilia hii, sasa ni wakati wa kujipa raha huku ukishuhudia jinsi watu wanavyoenda kuumbuka. Katika chuo anachosoma Celine, Marguel, Rio na Ethan, wanapangiwa safari ya kimasomo nje kidogo ya mji wa Manila.
Kwa bahati nzuri wazazi wote wa pande zote nne wanawaruhusu watoto wao kushiriki safari hiyo kwani ilikuwa ni muhimu sana katika kmasomo yao. Siku ya safari ikafika ambapo kwa Ethan ilikuwa ni kama vile ndoto iliyofika kabla ya siku zake kufika.
Celine anaonekana kuwa na wivu wa kimapenzi kwa wapenzi wawili, yani Margaux na Ethan ikiwa ni kutokana na mara kibao alivyokuwa akijifanya kuwa ni mpenzi wake Ethan ili kumnusuru rafiki yake Margaux asibambwe na mama yake Beatrice. Lakini kumbe Rio naye anaonekana kuwa na wivu kwa Ethan kwasababu ya Margaux.
Huku nuymbani kwao Margaux baba yake bado anaendelea na uchunguzi kwa mama yake Celine kwani alifanikiwa kugundua kuwa kunakitu Teresa amemficha, baada ya Teresa kumdanganya kuwa ile mimba aliyopewa na baba yake Margaux, baada ya kujifungua mtoto alifariki.
Kwaupande wa babu na bibi yake Margaux mambo yanzidi kuingiliana baada ya wazee hao wote kutuma watu wa kumperereza Teresa mama yake na Celine. Babu hataki kumsikia kabisa Teresa na Bibi anamtafuta binti yake Teresa ambaye hajaonana naye kwa muda mrefu.
Wivu unazidi kutanda kati ya Rio na Celine kwani kila mmoja natamani penzi la Margaux na Ethan, lakini kwa upande wa Margaux ameanza kuwashtukia. Margaux alimfuata Rio na kumuuliza, kulikoni siku hizi huongei sana na mimi wala huniambii matatizo yako kuna nini? Lakini Rio alificha hisia zake kwasababu kwa kiasi flani ameanza kuziweka kwa Celine.
Penzi la Ethan na Margaux bado linavikwazo kutoka kwa Beatrice mama yake na Margaux hata kwa Celine bado mambo ni magumu kwani mama yake hataki mwanae awe na urafiki na Margaux, kwani anahofia kuwa familia ya Margaux wakigundua siri ataambulia patupu.
Wakiwa huko safarini Ethan anawachukuwa Rio, Celine na Margaux wanaenda kuogelea, lakini waiwa huko, Margaux anazama katika kina kirefu cha maji, Celine anajitoa kumfuatilia ndani ya maji lakini alipomfikia mguu wake Celine ulikuwa umejinasa hivyo alishindwa cha kufanya. Lakini akiwa bado anatapa tapa Etnan na Rio tayari walikuwa wamekwisha wasiri, hivyo kila mmoja alimuokoa mwenzie.
Walimkimbiza Margaux hospitalini, na wazazi wa Margaux walikuja kwa hofu huku mama yake Margaux akimuwasha kibao Ethan baada ya kufahamu kuwa Ethan alikusika katika mchezo wa kuogerea. Nao wazazi wa Celine walipopata taarifa walikuja kwa hofu hadi hospitalini kumuona Celine. Lakini baada ya kumkuta Celine akiwa vizuri waliamua kumuondoa pale haraka haraka.
Wakati wakiondoka baba yake Margaux aliwaona kwa mbali Celine na mama yake, hivyo hofu ikamuingia na kutaka kumjua binti aliyoko na Beatrice. Sasa baba yake Margauxamekwisha fahamu kuwa Celine ni binti yake Beatrice ambaye huenda akawa ni binti yake aliyedanganywa kuwa alifariki akiwa mchanga. Je nini kitatokea endapo siri ikifichuka?
Fuatilia dondoo hizi hapa hapa Asili Yetu Tanzania Blog.

Hii tamthilia ni nzuri sana
ReplyDelete