Header Ads

Breaking News
recent

TAMTHILIA YA "HER MOTHER'S DAUGHTER" (Episode 6, 7 & 8) WASICHANA MAPACHA WAUNDA URAFIKI.

Margaux (kushoto) na Celine (kulia).
Wasichana mapacha wenye mvuto katika Tamthilia ya "Her Mother's Daughter" yani Celine na Marcue wanaendelea kunogesha mchezo, ambapo sasa Celine ameonekana kuwa mtatuzi wa matatizo ya msichana Margaux, na mpenzi wake Ethan.

 Celine anaonekana kuwa ni msichana mchangamfu asiyejifananisha na wasichana wenye maisha mazuri katika maeneo ya chuo. Kwakuwa Celine anafahamiana kidogo na Ethan mpenzi wake na Margaux, anagundua kuwa Ethan hana raha, hivyo anaamua kumuuliza kulikoni?.

Ethan anamuuliza "vipi wewe unaishi wapi?" Celine akatabasamu na kumueleza kuwa "bado sina sehemu maalumu ya kuishi hivyo nashindwa pakuanzia kutafuta" Ethan aliamua kwendanae kumsaidia kutafuta chumba. Lakini kabla hawajafika walipita sehemu kupata chakula, pale Ethan alimueleza Celine jinsi anavyoteseka na mapenzi ya Margaux. Celine alimpa mbinu mbali mbali za kukabiliana na hali hiyo.

Baada ya hapo Celine na Ethan waliondoka mpaka pale alipokuwa akiishi Celine na na kuamua kumpangishia chumba kwa siku ile. Ethan alifurahi kupata ushauri wa Celine kuhusu mahusiano.

Kama kawaida ya Celine kumchangamkia Margaux, siku moja Margaux, aliamua kumsikiliza Celine katika ushauri wake mzuri katika mambo mbali mbali, kwa mfano iposiku Ethan alipanga kuzungumza na Margaux, lakini walinzi walimbana sana kiasi cha kushindwa kufanya hivyo. Lakini Celine alibadilishana nguo na Margaux, akajifanya kukaa maktaba upande wa dirishani ili walinzi wamuone akiwa anasoma, lakini Margaux alikuwa akiongea na mpenzi wake Ethan. Kitendo hicho kilimfanya msichana Margaux, kumuomba urafiki Celine.

Margaux anamshawishi Celine wakalale wote kwao bila ya Beatrice mama yake Margaux kutarifiwa kuwa kunamgeni. Asubuhi ikafika, mara mama yake Margaux akaja kumuamsha aende chuo, lakini ile anafunua blanket alikutana na uso wa Celine, msicha ambaye ni mgeni katika uso wake.

Teresa mama yake na Celine waliamua kuhamia mjini anakoishi mwanae, kwani alishindwa kuvumilia kuishi mbali na mwanae. Hivyo walifunga safari yeye na baba yake hadi anakoishi mwanae Celine, lakini Celine hakuwa pale kwani alienda kulala kwa akina Margaux, hivyo walimpigia simu. Lakini mama yake Margaux, aliamua kumsindikiza Celine kwao kitu ambacho wamama hawa wawili ndugu wangekutana ingekuwa kasheshe. Lakini bahati nzuri walifika sehemu gari lao likashindwa kupita, hivyo Celine alishukia pale.

Wazazi wa Celine, yani mama, babu na binam walifanikiwa kupatanyumba ya kuishi baada ya  babu kuuza pete yake ya ndoa aliyofunga na mkewake ambaye alinyang'anywa na babu yake Margaux. Pia Celine anapewa msaada na rafiki yake Margaux, wa nguo na viatu. Wanakuwa marafiki na familia yake Margaux, wanampatia kazi ya kumfundisha binti yao Margaux.

Bado familia ya Ethan mpenzi wake na Margaux, inazidi kuletewa shida ya deni la babu yake na Margaux, analomdai baba yake Ethan. Baba yake haonekani alikojificha na Ethan anabeba mzigo wa majukumu ya nyumbani (mawazo mwanzo mwisho).

Babu yake Margaux, amkataza mjukuu wake kuwa na urafiki na Celine, kwani kunasiku walikutana njiani na Celine akamletea kasheshe, ikiwa ni pale ambapo babu yule alimlazimisha mwendesha baskeli alipe pesa kwasababu amekwaruza gari yake. Lakini kwa ujasiri Celine alimshushua yule babu pamoja na utajiri wake mpaka akaondoka, sasa fikiria anakutana naye kwa mwanae je inakuwaje?.. Kashe she juu ya kasheshe...
Fuatilia mwendelezo wa Tamthilia hii ya "Her Mother's Daughter" hapa hapa Asili Yetu Tanzania Blog.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.