WATANZANIA TUTEMBELEE VIVUTIO VYA UTALII WETU WA NDANI - HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI.
Hifadhi nzuri na zenye kuvutia mamilioni ya watu duniani wenye ndoto za siku moja kufika Afrika zinapatikana hapa kwetu Tanzania, japokuwa wengi wetu hapa nchini wamekuwa wakizembea kufanya utalii wa ndani.
Leo ikiwa ni siku ya utalii duniani, Tanzania tunazidi kuwavutia wageni wengi duniani kwa kuwa na vivutio vizuri pamoja na amani ya nchi. Wananchi walio wengi hatuna kitu kinaitwa time management yani jinsi ya kupangilia muda wakufanya mambo, kwa mfano muda wa mapumziko na kipindi cha kazi. Wenzetu wa majuu wanathamini sana mpangilio wa muda. Imefika wakati sasa tutenge hata muda kidogo wa mapumziko ya kutembelea vivutio vyetu vya asili ambavyo wazungu wanatenga madola miaka mingi ili kuja kutembelea mbuga zetu za wanyama.
Kufanya utalii wa ndani ni pesa kidogo tu, si sawa na mzungu anayetoka Ulaya au kwingineko duniani. Lakini chakushangaza utakuta kunamwananchi ambaye hajawahi kusikia hifadhi ya Mahale,au Tarangire hata Serengeti hajui iko wilaya gani! Tuthamini vya kwetu kwanza ili tuwape hamasa na wageni waweze kutembelea hifadhi zetu za Taifa.

Pundamilia |
HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, yenye ukubwa wa kilomita za
mraba 14763, ni Hifadhi ya pili kwa ukubwa nchini (baada ya Hifadhi ya Ruaha). Serengeti
ni moja ya Hifadhi maarufu sana duniani. Umaarufu wa Hifadhi hii unatokana na
misururu mirefu ya nyumbu wanaohama kwa makundi makubwa kutoka upande mmoja wa
mbuga hadi mwingine, na kuvuka mpaka wa Tanzania hadi hifadhi ya wanyama pori
ya Maasai Mara nchini Kenya. Wakichagizwa na mvua, kila mwaka zaidi nyumbu
milioni moja, pundamilia 2, 00,000, swala tomi 300,000 huunga msafara wa
kutafuta malisho na maji.
Hifadhi ya Serengeti, pia ni maarufu kwa wanyama walao nyama
chui na samba. Ukubwa wa hifadhi hii umesaidia
kudumisha uhai kulinda wanyama walio
hatari ya kutoweka kama faru weusi na duma. Katika Hifadhi hii
utashuhudia wanyama wawindaji kama duna wanavyowinda.
Aidha zipo aina zaidi ya 500 za ndege. Hifadhi ya Serengeti
ipo umbali wa kilomita 335 kutoka Arusha ikiambaa kaskazini katika mpaka wa
Kenya na Magharibi inapakana na Ziwa Victoria.Hifadhii inafikika kwa barabara
kutokae Arusha, Musoma, au Mwanza na vilevile kwa ndege za kukodi kutoka Dar es
salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha, Ziwa Manyara, na Ngorongoro.
Wakati mzuri wa kutembelea Hifadhi kuona uhamaji wa nyumbu
ni kuanzia Desemba hadi Julai; kuona wanyama wanaowinda Juni – Octoba. Kuna
maeneo ya malazi ndani ya hifadhi yenye hadhi tofautitofauti kama Hotel za
kitalii, kambi za kifahari, nyumba za wageni, hosteli ya wanafunzi na kambi
kadhaa za kupiga mahema ndani ya Hifadhi. Hotel zingine na kambi za mahema
hupatikana nje ya Hifadhi.
MAKALA HII IMEANDALIWA NA ASILI YETU TANZANIA.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA