WALANG HANGGAN (MY ETERNAL) DANIEL AZIDI KUSOTA JELA HUKU MIGUEL AKIHONGA WAFUNGWA WAMPIGE.
![]() |
Katika picha kushoto mtoto huyu ndiye aliyeigiza kama Daniel wakati akiwa mdogo, na kulia ni Daniel. |
Katika Tamthilia ya My Eternal, Daniel anazidi kusota jela baada ya mikakati ya Nathan ya kumsingizia kuwa ndiye aliyemchoma kisu tumboni na kutaka kumuua siku ya ugomvi wao, sasa inazidi kuchukua sura mpya baada ya kesi hiyo kuahirishwa mara kwa mara.
Dada yake Nathan yani Johana anasumbuliwa na nafsi yake baada ya kutunza siri nzito yenye ukweli wote utakaoweza kumsaidia Daniel kutokuhukumiwa kwenda jela. Tokea mwanzoni Johana alikuwa akimtaka Daniel kwa hali na mali lakini Daniel anampenda sana Katarina hivyo hakuweza kukidhi mahitaji ya Johana japokuwa bado anampenda sana Daniel.
Baada ya Johana kuona Daniel anasota Jela, anaamua kufuata huko huko jela na kuanza kumuomba msamaha, lakini Daniel anamwambia kwanini asiwaambie ukweli ili aondokane na kufungwa jela! Lakini Johana anamwaga machozi na kuzidi kuomba msamaha, kwani hawezi kufanya hivo na endapo akitoa ukweli basi kaka yake Nathan atakuwa katika wakati mgumu. Lakini Daniel anamwambia kuwa hata kama akimuomba msamaha mara milioni, kama asiposema ukweli ni kazi bure.
Baada ya Daniel kumpa kichapo Miguel huko jela, Miguel anampigia simu Thomas na kumuagiza amletee pesa nyingi na vyakula ili awahonge wafungwa wamtandike Daniel. Thomas namtumia box lililojaa mazaga zaga kibao anawagawia wafungwa wote, na kuwachochea wamfanyie mbovu Daniel.
Katarina na mama yake anahama nyumbani kwa Emily Gidoti na kurudi kwao kwa zamani ikiwa ni baada ya kumsikia Emily akimwambia Ihenya kuwa Katarina ndiye chanzo cha mwanae Daniel kuwekwa jela.
Nathan bado anazidi kupanga njama za kumteka Katarina, lakini Katarina anamuita Nathan mahali na kumuambia asipoteze muda wa kumfuatilia kwani uhusiano wake na yeye umekwisha, hivyo hawezi kuvunja uhusiano wake na Daniel.
Katarina anaonekana kutekwa kwa bastora na huko jela Daniel anapigwa vibaya takribani kupoteza maisha, je Daniel amefariki? Fuatilia dondoo zijazo hapa hapa Asili Yetu Tanzania.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA