TAMTHILIA YA KUSISIMUA YA WALANG HANGAN (MY ETERNAL) WIKI HII : DANIEL YUKO MAHUTUTI - ACHOMWA VISU KIBAO TUMBONI.
![]() |
Huyu ndio katarina anayewapagawisha Nathan na Daniel. |
Baada ya Miguel kupigwa na Daniel wakati wakigombana, sasa Miguel awahonga manyampala wa gerezani ili wamuuwe Daniel. Mbinu zinakamilika za kufanya tukio, siku hiyo Daniel alipangiwa kwenda kufanya usafi lakini wakati bado akiwa amejiinamia kitandani kwake, kunawafungwa wawili walikuja na kumkumbushia kuwa ilikuwa ni zamu yake na kama hawezi basi wamsaidie. Lakini Daniel alinyanyuka na kwenda kufanya usafi, ndipo Miguel na wafungwa wenzake walipomshambulia na kumchoma visu kadhaa tumboni na kumuacha akiwa ameloa damu sakafuni.
Akiwa chini ya sakafu huku akigugumia kwa maumivu makali alimuona baba yake Katarina ambaye alikwisha fariki kitambo, akimwambia "nipe mkono Daniel nitakusaidia usife" Daniel kwa maumivu makali alinyanyua mkono wake kwa tabu sana ili amshike mkono baba yake Katarina, laki mkono wake haukumfika kwani alishindwa. Kumekuwa na usemi kwamba, ukitokewa na ndugu yako usingizini wakati uko mahututi na alikwisha fariki na akakuomba mkono au kukuita, ukimfuata basi hutopona nawe utakufa, na huenda usemi huu ndio alioutumia Daniel.
Polisi wanampigia simu baba yake Marco Montenegro baba yake Daniel na kumpa habari mbaya za kushtusha, kuwa Daniel amechomwa visu. Na baada ya hako anapigiwa simu Emily Gidoti mama yake Daniel baada yakupokea ujumbe huo mzito, anabaki mdomo wazi. Kisha ujumbe ukazidi kuenea, kwani Miss Ihenya naye alimpigia simu Katerina na kumpasha habari hivyo Katerina naye alijikuta akimwaga machozi.
Wahusika wote wa Tamthilia ya Walang Hanggan walijikuta wakikutanika hospitalini bila kujali tofauti zao za kila siku. Walipofika hapo Daniel alikuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ambapo alipoteza fahamu kabisa na kuanza kushtuliwa na zile shoti za kumshitulia mtu aliyezimia, lakini ilikuwa ngumu kwa Daniel kuzinduka.
Kabla ya hapo Thomas amefuatwa na mama yake mzazi akimuomba msamaha amsamehe lakini Thomas anamkana na kumwambia kwanini aliwakimbia na kwenda kwa mwanaume mwingine? Huenda angemfikilia kumsamehe ndapo angekuwa amefariki kabisaa! Thomas anamfukuza mama yake na anamwambia hataki kumuona.
Nathan naye anaonekana kumteka Katarina lakini anamuacha baada ya Katarina kukubaliana naye kuwa atarudiana nae. Lakini siku iliyofuata Walikutana tena siku hiyo ilikuwa kasheshe kwani Katarina anamuomba Nathan asiendelee kumfanyia unyama Daniel bali aseme anachotaka naye atafanya. Nathan anaonekana kutabasam na kumpa masharti matatu Katarina. Moja ni kufuta kesi yao ya taraka, pili kuwatangazia watu wengi kwa pamoja kuwa alifanya kosa kuachana na Nathan, na tatu wafunge ndoa upya.
Katarina kabla ya kukubali alibadili mawazo na yeye kumpa masharti Nathan, moja ni kumfutia kesi Daniel ili atoke jera na mbili ni kuweka ukweli wazi. Masharti hayo yanamchafua roho Nathan na kukiri hatoweza, naye Katarina anasema kama hutoweza basi masharti yako sitayafanya pia.
Johana anaonekana kuwa na wasi wasi baada ya kuwa na siri nzito juu ya kumsingizia Daniel na kuweka lumande. Johana anamwambia Nathan lazima niseme ukweli kabla Daniel hajafa, asijekufa na damu yake ikabaki juu ya mikono yangu. Nathan anamtishia Johana lakini Johana naye anamtishia kuwa atamshawishi Katarina aseme kuwa Nathan alimbaka.
Baada ya Marco Montenegro na Emily kujua kuwa Miguel ndiye aliyehusika katika mpango wa kumchoma visu Daniel basi wanamfuata Miguel jela na kumpa kipigo mbele ya maaskari. Lakini baada ya hapo Marco Montenegro anaonekana kutekwa na watu wasiojulikana, je ninani hao?. Huko chumba cha wagonjwa mahututi, Daniel anarudiwa na fahamu. Nathan anamfuta Miguel jela na kumtaka amuuwe Daniel alafu yeye atamlinda Emily ili asiolewe na baba yake "Marco Montenegro". Je nini kitaendelea? Karibu Asili Yetu Tazania blog.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA