MAUWAJI KENYA IDADI YAFIKA 59 YA WALIOUWAWA NA WENGINE WAKITEKWA.
![]() |
Baadhi ya watu waliokuwemo katika jengo lililoshambuliwa, wakiokolewa na polisi. |
Serikali ya Kenya kupitia kwa waziri wake wa usalama Joseph
Ole Lenku imesema kuwa watu 59 wamefariki katika shambulizi la kigaidi
lililofanywa na wanamgambo wa Al Shabaab na wengine 175 kujeruhiwa.
Waziri Ole Lenku amesema kuwa idadi ya magaidi walio ndani
ya jengo hilo ni kati ya kumi na kumi na tano na haijulikani ikiwa wanwazulia
waathiriwa au waathiriwa wamjificha katika sehemu mbali mbali z jumba la
Westgate.
Shirika la Red Cross awali katika taarifa yake ilisema kuwa
watu 43 ndio waliofariki na zaidi ya 50 kujeruhiwa huku wengine wakitekwa nyara
katika mashambulizi la kigaidi Jumamosi mchana.
Milio ya risasi imeweza kusikika katika jengo la Westgate
mjini Nairobi Kenya, ambako wanamgambo wa Al shabaab wanawazuilia mateka ambao
idadi yao haijajulikana hadi sasa.
Wanajeshi wawili walijeruhiwa katika ufyatulianaji huo na
kukimbizwa hospitalini kwa matibabu huku watu wawili wakinusuriwa asubuhi ya
leo.
Hadi sasa jeshi limeweza kudhibiti hali nje na ndani ya
jengo hilo, magari ya kijeshi yakiwa yameletwa katika eneo hilo huku polisi na
wanajeshi wakijaraibu kuwanusuru baadhi ambao wangali wanazuiliwa ndani ya
jengo hilo.
Watu 39 wameuawa baada ya wanamgambo hao kushambulia jengo
hilo mwanzo katika eneo la kuegeshea magari na kisha kuingia ndani ya mikahawa
na maduka katika jengo hilo lenye ghorofa nne na kuwpaiga watu risasi kuholela.
Kuna taarifa kuwa wanamgambo hao wako ndani ya duka moja
kubwa katika jengo hilo.
Rais Kenyatta anasema kuwa baadhi ya waliofariki ni jamaa
zake. Miongoni mwa waliofariki pia ni mwanadiplomasia wa Canada na raia wawili
wa Ufaransa. Rais Kenyatta anasema kuwa wale waliohusika lazima wakabiliwe na
mkono wa sheria.
Jamaa na marafiki waliofika kujua hali ya jamaa zao wamezuiwa
kuingia ndani ya jengo hilo. Wengi wa waathiriwa walifariki kutokana na
majeraha yao.
Source: BBC
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA