Header Ads

Breaking News
recent

"JAY Z NA BEYONCE" WAONGOZA "FORBES" - MASTAA WANANDOA WENYE KIPATO KIKUBWA KWA MWAKA 2013.

 Kwa mujibu wa takwimu za Forbes zinazotolewa kila mwaka katika categories mbali mbali, leo takwimu hizi zimevunjwa na mastaa wawili wanandoa yani Beyonce na Jay Z ambao ndio wanandoa wanaoongoza kwa kuingiza mapato makubwa kwa mwaka 2013. Mastaa hawa tokea mwezi Juni 2012 hadi mwezi Juni 2013 wameingiza dola milioni 95.

Nafasi ya pili ilikamatwa na Tom Brady na Gisele Bundchen, wao kwa pamoja kwa muda wote huo wametengeneza dola milioni 80.

Nafasi ya tatu ilishikwa na Angelina Jolie na Brad Pitt na wao walitengeneza milioni 50. Na nafasi ya nne ilichukuliwa na Ashton Kutcher na Mila Kunis ambapo wao walitengeneza dola milioni 30.

Mastaa wengine walioingia katika top 5 ya Forbes ni Kanye West na Kim Kardashian ambapo wao walishika namba tano. Kim Na Kanye wao walitengeneza dola milioni 30.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.