MICHELLE OBAMA KUACHIA ALBUM YA MUZIKI WA HIP HOP.
Mke wa rais wa Marekani Michelle Obama ameanza kuachia baadhi ya nyimbo za hip hop zitakazo unda album ya muziki inayolenga kuwaasa watoto wa Marekani kuhamasika kufanya mazoezi na kufanya uchaguzi mzuri wa vyakula ili kuepukana na afya uzembe yani vitambi.
Michelle kwakushirikiana na shirika la Afya la marekanai na "taasisi wazi ya afya ya hip hop" wataachia nyimbo 19 zitakazo unda album hiyo inayoitwa "Songs For a Healthier America". Michell katika kuendeleza kampeni yake ya "Lets Move" tayari amekwisha achia wimbo mmoja wa video unaoitwa "Every body" ambapo Jordin Spark ameshirikishwa mle.
Album hiyo itakuwa ni ya video ambapo ndani yaka hutamuona Michelle akiimba japokuwa ataonekana katika nyimbo hizo. Times Magazine imezidi kufunguka kuwa, wamekwisha achia wimbo wa video unaoitwa "Every Body" utazame hapo chini.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA