SHEHENA YA MABOMBA YA GESI YA MTWARA KWA AWAMU YA KWANZA YAPOKELEWA NA WAZIRI MKUU. (ITV HABARI)
Waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda amepokea shena ya kwanza ya
mabomba kwa ajili ya ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka Mtwara na Songo
songo hadi Dar es Salaam huku akiwataka wanachi kutoa ushirikiano wa kutosha
ili kufanikisha mradi huo ambao una tija kubwa kwa uchumi wa taifa. Mh Pinda
amepokea shehena hiyo katika bandari ya
Dar es Salaam ambapo amesema inashangaza kuona baadhi ya watu kwa makusudi
kabisa wanapotosha ukweli wa mambo kuhusu mradi huo.
Awali wakizungumza kuhusu mradi huo waziri wa nishati na madini Mh profesa Sospeter Muhongo
amesema sasa serikali imeanza safari ya
maendeleo wakati mkurugenzi mtendaji wa shirika la maendeleo ya petrol nchini
TPDC Bw Yona Kilagane amesema hiyo ni
awamu ya kwanza ila zinakuja jumla ya meli 12 zenye shehena hiyo.
Kwa upande wa balozi wa China hapa nchini Dk Lu Youging
ambao ndio wajenzi wa mradi huo wamesema
wataendeleza mahusiano mema ambao yamekuwepo kati ya China na Tanzania
kwa muda mrefu huku akitolea mfano ujenzi wa reli ya Tazara.
Chanzo cha habari: ITV TANZANIA
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA