MWANARIADHA MAARUFU WA TANZANIA - "BOAY AKONAAY" AFARIKI DUNIA GHAFLA".
BOAY AKONAAY amefariki dunia ghafla juzi nyumbani kwake Njiro mkoani Arusha, ambapo hadi akifikwa na umauti alikuwa bado muajiriwa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Katika historia ya BOAY alikuwa ni mwanariadha wa mbio ndefu aliyezaliwa mwaka 1970 katika kijiji cha BASSOTU Wilaya ya HANANG mkoani MANYARA, ambapo alikulia katika kijiji cha DUMBETA na kusoma shule ya msingi KATESH (Bweni) . Boay alikuwa ni mtoto yatima ambapo alitunzwa na baba yake mdogo, huku akisomeshwa na mwalimu aliyeitwa SAMAITU.
AKONAAY ni jina alilorithi kutoka kwa baba yake mdogo aliyemlea ambapo baba yake mzazi anaitwa mzee KAWA ambaye alikwisha tangulia mbele za haki miaka iliyopita.
AKONNAY alikuwa ni mwanariadha mahiri kutoka wilayani Hanang, ambapo anaunga orodha ya wanariadha wengi akiwemo Gidamis Shahanga, Alfredo Shahanga, Simon Robert (ni marehemu), Andrea Sambu,Thomas Naali, Gewai Suja Francis Naali, John Nada Saya (ni marehemu) na wengine wengi.
ASILI YETU TANZANIA inawapa pole ndugu jamaa na marafiki katika kuondokewa na mpendwa wao bwana BOAY AKONAAY. Pia Site hii inamshukuru mwanariadha wa zamani bwana WILHELM GIDABUDAY kwa ushirikiano aliyotoa katika kuandaa habari hii.

HAYA NI BAADHI YA MAFANIKIO ALIYOLILETEA TAIFA LA TANZANIA.
ASILI YETU TANZANIA inawapa pole ndugu jamaa na marafiki katika kuondokewa na mpendwa wao bwana BOAY AKONAAY. Pia Site hii inamshukuru mwanariadha wa zamani bwana WILHELM GIDABUDAY kwa ushirikiano aliyotoa katika kuandaa habari hii.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA