TAMKO LA WANAHABARI KATIKA UZINDUZI WA AZIMIO LA KUWALINDA WAANDISHI WA HABARI WANAPOKUWA KAZINI.
Kufuatia Mkutano wa Wadau wa Habari Afrika Mashariki
waliadhimia yafuatayo;-
1.Serikali zote nchi za Afrika Mashariki zihakikishe kuwa
Katiba za nchi zao zinakuwa na vipengele kwa ajili ya:
-Kuwa na tasnia ya habari ambayo ipo huru, salama na yenye
kujitegemea ikijumuisha usalama wa wanahabari.
-Sheria nyingine zote ziheshimu Katiba za nchi zikiendana na
vyombo na mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu.
2. Wamiliki wa vyombo vya habari wafanye marekebisho ya
miundo ambayo itazingatia yafuatayo;
- Uendeshaji bira- Ikiwa ni pamoja na masuala ya Ajira,
Mishahara, Mikataba, Motisha na Marupurupu mengine ya kifedha.
- Viendeshwe kwa kufuata na kuheshimu miiko ya Kitaaluma.
-Kuhakikisha kuwa wanahabari wote wanakuwa na Bima.
-Vyumba vya habari viongeze uwekezaji katika mitandao ya
kijamii pamoja na utoajji elimu kwa wanahabari kuhusu mitandao binafsi yaani
Blogs.
3. Baraza la Habari lishirikiane na taasisi na vyama vya
kitaaluma vya wanahabari ili kudumisha na kulinda ueledi na umoja katika tasnia
ya habari.
4. Wanahabari waanzishe vyama vya wafanyakazi ili kuwezesha
na kuongeza mapatano na makubaliano ya hiari sehemu za kazi.
5. Wamiliki wa vyombo vya habari walinde na kutetea usalama
wa wanahabari na vyombo vyao kupitia
-Wamiliki wa vyombo vya habari kuweka na kuzingatia taratibu
za usalama sehemu za kazi
-Wamiliki wa vyombo vya habari wahakikishe wanwapatia
waandishi wa habari vifaa vya usalama au vya kujikingia na hatari na wawezeshe
mafunzo juu ya taratibu za usalama.
-Kujumuisha mitaala ya mafunzo ya usalama na ulinzi katika
taasisi zote za mafunzo ya uandishi wa habari.
- Wanahabari wao binafsi wachukue vipaumbele na tahadhari
katika usalama wao binafsi.
6. Jumuiya ya Afrika Mashariki lizitake nchi wanachama wake
ambao walitia sahihi itifaki ya Udhibiti wa Tovuti wajiondoe katika Mkataba huo
ikiwa ni njia moja wapo ya kudumisha utawala bora na uwajibikaji.
7. Serikali za Afrika Mashariki zifanya juhudi katika
kuwezesha uanzishwaji wa mfumo wa kisheria wa kuruhusu uendeshaji bora wa
mitandao ya kijamii na wakati huo huo wakilinda uhuru wa wadhibiti ili
kuboresha na kuendeleza uhuru wa mitandao ya kijamii katika eneo la Afrika
Mashariki.
Source: Libeneke la Kaskazini


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA