PICHA ZA RAIS OBAMA NA FAMILIA YAKE WALIPOTEMBELEA KISIWA CHA GEREZA LA "ROBBEN" ALIPOKUWA AMEFUNGWA "NELSON MANDELA" WAKATI WA KUPINGA UBAGUZI WA RANGI.
Rais wa Marekani Barack Obama akitazama chumba namba 5. katika gereza la Robben ambamo katika chumba hiki ndimo Rais wa zamani wa Afrika kusini Nelson Mandela alipofungiwa kwa miaka 18 kati ya miaka 27 aliyofungwa jela. (AP Photo/Carolyn Caster)
Rais Obama akiwa na mke wake Michelle Obama siku ya Jumapili ya tarehe 30 wakati walipotembelea Gereza la Robben lililoko kisiwani ambako Mandela na wenzake wapigania haki za kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini walikofungwa hapa. (AP Photo/Evan Vucci).
Rais Obama na familia yake pia walitembelea "rock quarry" sehemu ambako Nelson Mandela na wafungwa wenzake walipokuwa wakilazimishwa kufanya kazi katika eneo hilo lililoko ndani ya kisiwa cha Robben. (AP Photo/Evan Vucci).
Kutoka kushoto ni Michelle Obama, Sasha Obama, Ahmed Kathrada mfungwa aliyekuwa pamoja na Nelson Mandela Gerezani kwa miaka 18 kati ya miaka 27 aliyofungwa Mandela, Rais Barack Obama, Marian Robnison na Leslie Robinson. (AP Photo/Carolyn Caster).





No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA