TAMTHILIA YA “WALANG WANGGAN” EPISODE YA 1&2 – MAHUSIANO YA “MARCO” NA “EMILY” YAWEKEWA VIKWAZO.
Baada ya Mara na Clara kufanya vizuri, sasa ni Emily na Marco ambao wanatokea
kupendana na kulishana viapo vya kuto umizana katika mahusiano yao. Lakini mama
yake MARCO tayari ameanza kuweka vikwazo kibao.
MARCO ni kijana pekee anayetoka katika familia ya kitajiri ya
mzee Joseph huku mama yake anaitwa “Margret”.
Marco anatokea kumpenda mmoja wa watumishi
wa mama yake anayefahamika kama EMILY.
EMILY ni binti anayetoka katika familia masikini, huku akiwa
akiishi na baba yake. Emily ni mfanyakazi wa familia ya MARCO. Siku moja familia ya Marco waliaandaa sherehe
nyumbani kwao na kuwaalika watu wengi katika sherehe hiyo huku Emily akiwa
mmoja wa wahudumu.
Emily akiwa amebeba vyakula akipeleka katika sherehe, mara
alimuona Marco akikatiza kwa mbali, alikuwa kama amepigwa na butwaa kidogo huku
akiendelea kujongea. Wakati akiliopogeuka tu wakagongana na mama yake Marco
ambaye ni boss wake, alikasilika sana kwani alionekana kuaibika mbele.
Siku Marco anaenda kumtambulisha Emily kwa mama yake,
ilikuwa tofauti kwani mama yake alimkatalia Marco kutaka kumuoa Emmily, kwani
aliamini kuwa Emily amempenda Marco kwasababu ya pesa alizonazo.
Tayari Margret mama yake Marco anatinga nyumbani kwao Emily
na kumuachia vitisho kibao ikiwemo kunyang’anywa ardhi yao.
Baada ya mama yake Marco, kuiandama familia yao Emily, sasa baba
yake Emily anaamua kuondoka na binti yake
katika mji jirani ili kuepukana na zahama ya Margret. Lakini mama yake Marco
anamtuma mtu awafuatilie na kuwabambikizia uzushi ili baba yake Emily awekwe
jela.
Mtu aliyetumwa anafanikiwa kufanya hivyo, isipokuwa inakuwa
kinyume, kwani baba yake Emily wakiwa
mahakamani anaanguka na kuzimia, matokeo yake Emily ndiye anapelekwa jela
ambapo alionekana ni mja mzito baada ya siku chache kufika jela.
Mipango yote hiyo ya Margret, Marco hakujua napia hakujua
kama Emily alikuwa na mimba yake, sipokuwa alipata taarifa ya Emily kuwa jela
ambapo aliweza kumtembelea, lakini Emily alimtimua.
Marco na Jenny wanafunga ndoa baada ya Emily kumsusia Marco,
huku Emily anajifungua mtoto wa kiume ambae inasemekana amefariki mara baada ya
kuzaliwa. Je, kunaukweli wowote kuhusiana na motto kufariki au ni kiini macho
tu?
Je nini
kitaendelea? Karibu tena kwa dondoo nyingine za tamthilia hii hapa hapa.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA