TAMTHILIA YA “MARA CLARA” EPISODE 58: “GARY” ATOROKA JELA NA KUMTEKA “ALVIRA”, HUKU “AMANTE” ANUNUA BASTOLA (VITA INAANZA).
Mchongo wa Familia ya Amante kutaka kuhamia Dubai, ambako
ndiko Amante alikuwa amepata kazi baada ya misuko suko mingi iliyoikumba
familia yake na kujikuta akifirisika, ulipelekwa jela na Clara ambae alimwambia
baba yake Gary aliyekuwa jela kuwa Alvira na familia yake wanataka kuhamia
Dubai. Gary kusikia hivyo kwakuwa anampenda Alvira, aliamua kupanga mbinu za
kutoroka jela na kuja uraiani.
Baada ya Gary kufanikiwa kutoroka jela, anamteka Alvira na
kumficha pasipojulikana, huku akimlazimisha akubali kuwa anampenda yeye na sio
mumewe Amante.
Gary pia anapanga njama nyingine na kumlipa mtu akamuue MARA
na Amante. MARA na Christian wakiwa njiani katika harakati za kumtafuta Alvira, jambazi anatokea na gari moja dogo
jeusi na kumshuti MARA,lakini anamkosa.
Kumbe Amante alikuwa mbele ya lile gari, naye alijibu mashambulizi ya risasi
kwani naye amenunua bastola kutokana na maudhi ya Gary. Amante anafanikiwa
kumteka jambazi na kumkabidhi kwa maskari.
“MARA” anazidi kuwa na wasi wasi na Clara huenda akawa nahusika katika mkakati
wa kumteka mama yake Alvira. Anaamua kwenda nyumbani kwa akina Clara na
kumuuliza ni kwanini yeye hajishughurishi katika kumtafuta mama yao? Clara
anashindwa kujibu na kuamua kuanza kupigana, wakiwa wanapigana mama yao Suzan
anawaachanisha.
Clara anaamua kwenda alikotekwa Alvira, na kujionyesha kuwa
anahusika pia katika utekaji huo. Alvira analia kwa uchungu akimuuliza Clara,
nikwanini nayeye ameamua kumfanyia hivo. Lakini Clara kwa ujasiri alijibu “wewe
si ulinisaliti na kumchagua MARA kuwa ndiye unayempenda?”
Siku iliyofuata baada ya Clara kukwaruzana tena, mama yake
Clara “Suzan” alimuamru MARA aondoke, MARA aliamua kuingia mtaani, akiwa
anashangaa shangaa, mara akamuona Clara anakatiza mtaani. MARA anaamua kumfuata
Clara kwa nyuma nyuma hadi anafanikiwa kuingia alikofungiwa mama yake “Alvira”.
MARA anamnyanyua mama yake ili watoroke, lakini kabla ya
kutoroka , alimpigia simu baba yake na kumuambia maeneo waliko. Akiwa bado
anaongea Gary na Clara waliingia na kuwanyang’anya simu na kuwafunga kamba.
Kutokana na kila wakati Clara na MARA wanapokutana lazima wapigane, sasa Gary
anaamua kumfungia MARA kabatini.
Muda mfupi polisi wanafika eneo hilo, Gary anajidai kumteka
mwanae Clara kwa kumuwekea bastola kichwani, na endapo polisi wakijaribu
kumsogelea, basi atamripua. Akiwa bado amemshikilia Clara mara risasi inapigwa.
Je, ninani kapigwa? Gary au Clara? Na kama sio hivyo, Gary atamripua Clara?
Je nini kitaendelea? Tazama Star TV kila J4, IJumaa, Jumamosi,Juma Pili
– saa tatu usiku na karibu tena kwa dondoo
nyingine za tamthilia hii hapa hapa.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA