Header Ads

Breaking News
recent

MSIBA WA MSANII "NGWEA" TARATIBU ZAANZA KUPANGWA NA BABA YAKE MDOGO.

Baba Mdogo wa Marehemu Mzee Mangwair ambaye yuko Mbinga Songea kikazi, amesema kuwa wamekubaliana na kaka yake mkubwa yaani Baba Mkubwa wa Ngwair, David Mangwair ambaye naye yuko Songea kuwa watu watakutanika Mbezi kwa msiba na pia mapokezi yatafanyika hapa Dar es salaam Mbezi Beach.
Ingawa bado kikao cha familia nzima hakijafanyika lakini Baba huyo mdogo amesema wanaweza kulazimika kuzika Morogoro sehemu ambayo baba yake alizikwa.

Baba huyo mdogo alisema kuwa kesho ndo watarudi Dar es Salaam pamoja na Kaka yake yaani Baba Mkubwa wa marehemu.Kuhusu mwili kuletwa hapa Tanzania kutoka Africa ya Kusini Baba mdogo amesema kuwa mpaka sasa hawajajua jinsi gani mwili hup utafika hapa lakini kuna ndugu zao ambao tayari washaanza kufanya taratibu za kuwasiliana na Ubalozi wa Africa ya Kusini ili kujua ni jinsi gani mwili huo utafika hapa.

Kama kutakuwa na mabadiliko yeyote watakapowasili kesho Baba mdogo na Baba Mkubwa baada ya kikao cha familia watatoa taarifa.


Na - Annapita.com

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.