Header Ads

Breaking News
recent

HATIMAE MISS SERENGETI 2013 APATIKANA.


Huyu ni mshiriki anayejulikana kwa jina la "Imelda Joseph" aliyekuwa na namba ya ushiriki nne.

Mashindano hayo yalifanyika usiku wa tarehe tatu mwezi wa nne 2013 katika hotel ya Giraffe katika mji wa Mugumu Wilayani Serengeti. Mshiriki huyo ni mfanyakazi wa "Newsland Barber Shop" ameweza kujinyakulia taji hilo na kitita cha shilingi laki tatu tasilim pamoja na zawadi kemkem.

Pia shughuli hiyo ya kumtafuta mlimbwende huyo iliongozwa na shoo za wasanii mbalimbali akiwemo H.BABA aliyesindikizwa na wasanii kibao wa Wilayani hapo, kweli ilifana sana.

Pongezi kwa SHANYANGI GENERAL SUPPLY NA WENZAKE WOTE WALIOFANIKISHA ZOEZI HILO .

Credit to - Alphan Nyaga.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.