TAMTHILIA YA “MARA CLARA” EPISODE YA 44 KIFO CHA “MARA” SIRI NZITO YA ANZA KUFICHUKA.
![]() |
CLARA NA MARA |
Polisi wanaenda kumkamata Christina, mara anafanikiwa
kuwachenga, wakati anatoka nje ya ofisi yake, Gurlly anatokea na gari huku
amevaa mask na kumchukua. Gurlly anamficha sehemu, huku akipanga njama za
kumkamatisha mauwaji ya “Mara”
Avira amcharukia Amanthe baada ya kuambiwa kuwa Christina
ndiye aliyepanga njama za kumuua mwanae, lakini kwa upande wa Clara bado
anatumia mwanya huo kuwa na mama yake wa zamani (Avira).
Christian anamuomba mama yake ruhusa na kuamua kwenda mbali
kidogo na mji, kule ni kwandugu yake. Kumbe wakati Christian akiwa mdogo alikuwa anaitwa “Uttoi”.
Christian ameamua kuitembelea familia iliyomlea huko kijijini, kumbe Christian
ndiye pia aliyemuokota Mara, baada ya bomu kuripuka “Mara” alimpigia simu na
kumpeleka huko. Christian amkuta Mara pale kwao kijijini na anajifanya hamjui.Baadae
wanakaa pembeni na kukumbukana vizuri.
Huko nyumbani kwa Gurlly maelewano hakuna kwani Clara
amemcharukia ile mbaya, kwa mauwaji aliyofanya kwa “Mara”.
Avira atibuana na mama yake Gurlly kwani alienda kumtembelea
Clara, mama yake Gurlly hataki kumuona Avira akienda pale, lakini Avira apata
nafasi ya kutoka out na Clara.
Christina ampigia simu Amanthe na kumuambia kama atapelekwa
jela basi atamripoti polisi kuwa alitumia pesa za kampuni vibaya kwahiyo naye
ataenda jela, lakini Avira anasa mazungumzo yao na kuonekana kupunguza jazba
kwa mumewe huenda amemsamehe.
Mama yake Gurlly amegundua mchezo wa Gurlly kumficha
Christina, kwani amemfuatilia hadi alikomficha na kumuona Christina kwa macho.
Sasa bibi huyo aamua kwenda kwa Amanthe na kuonekana kunajambo anataka
kumuambia.
Nini kitaendelea, tazama Star TV na karibu tena kwa
dondoo nyingine za tamthilia hii hapa
hapa.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA