TAMTHILIA YA “MARA CLARA” EPISODE 48 NA 49 – MAJAMBAZI WAZIDI KUIVAMIA NYUMBA YA AMANTE NA MKEWE ALVIRA, WATAKA KITU.
![]() |
| CLARA NA CHRISTIAN (PICHA) |
Katika Tamthilia iliyopita Garl anaonekana kuzidisha ukatili
dhidi ya Amante, kwani afanikiwa kumtupia kisanga kinachompeleka lumande moja
kwa moja.
Christina ampigia simu Amante na kutaka kuueleza ukweli,
lakini Gary ashtukia mchongo huo na kumtangulia Amante kufika kwa Christina na
kumnyonga hadi kifo. Baada ya Gary kufanya mauwaji hayo anatoroka na kumuacha
Amante akiwasili kwa Christina na kumkuta akiwa tayari amekwisha fariki dunia.
Akiendelea kushangaa mara polisi wanafika na kumtuhumu kuwa ndiye aliye muua
Christina.
Suzan afanikiwa kutoroka na kukutana na MARA watoroka,
lakini Gary ashtukia na kuagiza watu wawafuatilie na kuwakamata lakini wanapigwa
chenga na basi kuondoka kusiko julikana.
Gury anawatuma majambazi wawili kuvunja nyumbani kwa Alvira
ikiwa ni mpango wake wa kufanya Alvira aogope na kumuomba msaada ili ammtie
mikononi mwake.
Gary anaanzisha mazoea ya kwenda nyumbani kwa Alvira
akijifanya anawapa ulinzi na msaada wowote watakaohitaji. Alvira anamua kupatia
kazi ya udereva katika kampuni yao lakini Clara anaonyesha wasiwasi na uamuzi
huo.
MARA na Suzan wafanikiwa kupata kazi katika Lordge moja huko
walikofikia, pia Alvira amepigiwa simu na Suzan kumueleza kuwa huko waliko
wanaendelea vizuri, lakini wakiwa bado wanaongea Clara anafika, Alvira
anabaki mdomo wazi.
Gary anatumiwa Ujumbe wa vitisho nyumbani kwake lakini
anamtuhumu Christian kuhusika na vitisho hivyo. Gary anaamua kuuchukuwa Ujumbe ule
hadi jela aliko Amante na kumpatia Ujumbe ule akidai kuwa “nakurudishia Ujumbe ulionitumia”.
Amante anashangaa na kuukana lakini anacheka na ku muambia Gary kuwa “huenda
kuna mtu anajua mkanda mzima wa maovu yako ndo maana anafanya hivi, lakini
sitakoma kufuatilia ukweli hadi nihakikishe maovu yako yanafichuka”.
Gary akiwa bado anatafakali ninani anayemfuatilia wakati
anafika nyumbani anakuta bahasha na kuifungua. Ndani yake anakutana na picha
zake akiwa na majambazi wake huku akiwa ameshikilia bastola. Lakini paia
kunawatu wanazidi kumfuatilia na ripoti hiyo imeonekana inapelekwa kwa Alvira.
Alvira anaamua kwenda kumsalimia mama yake Gary, lakini bibi
huyo anaonekana kuwa na jambo la kusema. Alvira anampa karatasi na bibi huyo
kumuandikia maneno yakiwemo kuhusu pesa na uovu wa Gary. Lakini kwa bahati
mbaya Alvira anaisahau karatasi ile chini na Gary kuikuta, anahaha na kuongea
kwa ukali akimuuliza mama yake “pesa zangu zikowapi??”
Familia ya Amante akiwemo Yule bibi wa kazi wavamiwa na
majambazi tena, lakini pia kwa upande wa Christian yuko hatalini kwani Gary
amesema akibaini ndiye anayetuma watu basi utakuwa ndio mwisho wake.
Je nini kitaendelea? Tazama Star TV na karibu tena kwa
dondoo nyingine za Tamthilia hii hapa
hapa.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA