PICHA: HUYU NDIYE "SIZE 8" MSANII WA NYIMBO ZA KIZAZI KIPYA ALIYEOKOKA - KENYA.
Mwimbaji wa
Muziki wa kizazi kipya Nchini Kenya Linet Munyali a.k.a Size 8,
ametangaza rasmi ya kuwa Ameokoka na hivyo kuachana na Muziki wa Kizazi
kipya.
Akiongea na Mtangazaji wa Clouds Fm
Millard Ayo kupitia kipindi cha Amplifier April 12, Size 8
alisema, "Nimeamua kuokoka kwasababu Maisha yangu yalikuwa hayana Amani.
Mara nyingi nilikuwa Mtu wa Huzuni na kuna kipindi nilikuwa nikitoka
kufanya Show Usiku najikuta nalia mwenyewe".
"Pamoja na kwamba pesa ninayo lakini
maisha yangu yalitawaliwa na Huzuni" aliongeza Size 8. Akitoa sababu ya
yeye kutokuwa na Amani, Size 8 amesema kuwa, hali hiyo ilikuwa ikimtokea
tu, na yeye pia hajui sababu ilikuwa ni nini.
Huyu atakuwa si Mwimbaji wa kwanza wa
Muziki wa kizazi kipya Nchini Kenya kutangaza kuokoka. Mwimbaji mwingine
aliyewahi kuokoka ni DNA aliyetamba sana na Wimbo wa Banjuka. Kwa
Tanzania Mwimbaji Stara Thomas pia aliwahi kutangaza kuokoka lakini
akaamua kurudi nyuma tena na kuimba Bongo Flavour tena.
Swali la Msingi la kujiuliza, ni; Je!
Nini kinafanya Waimbaji hawa kurudi nyuma na kuimba tena Bongo Flavour?
Ni jukumu la Kanisa sasa kuhakikisha kuwa watu kama hawa wanalelewa
vizuri Kiroho ili waweze kudumu katika Wokovu.
Chanzo: Gospel News Media

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA