Header Ads

Breaking News
recent

NDANI YA EPISODE YA 47 YA TAMTHILIA YA "MARA CLARA" - "MARA" AZIDI KUTAFUTWA KILA MAHALI.


"GARL NA CLARA"
Vina saba (DNA) vyaonyesha kuwa waliomzika sio MARA ni Lenita, lakini bado hali ni tete kwani Garl anadai akimuona MARA atampoteza kwa mikono yake mwenyewe.

Christian afanikiwa kumuhamishia MARA katika nyumba nyingine, lakini Garl apata mchongo kutoka wa Clara kuwa huenda Christian akawa anajua sehemu MARA alipo. Garl anamfuatilia Christiani hadi nyumba alipomficha MARA, lakini Garl anashindwa kung’amua siri hiyo na kuamua kumtumia mtu mwingine ili aendelee kuchunguza nyumba hiyo. Jambazi huyo akiwa nje ya nyumba alimo MARA ikiwa ni mida flani ya usiku, ghafla Christian anajitokeza na bonge la camera na kumpiga picha Yule jambazi.

Baada ya familia ya Amante kupata uhakika kuwa motto wao Mara bado yuko hai, waliamua kuchapisha picha za MARA na kuzisambaza kwa kila mtu ili kubaini alipo MARA. Wakiwa katika zoezi hilo walifika katika duka moja la mama mmoja ambaye kwa mara ya kwanza MARA aliponusulika kwa bomu alifika pale na kumuomba apige simu huku sehemu ya uso wake ukiwa unavuja damu – mama Yule aliwapa Ujumbe huu wazazi wa MARA (Amante na Alvira).

MARA azidi kumtembelea bibi yake kwa siri, japokuwa bibi huyo anamengi ya kumuambia lakini anashindwa kwa sababu ya ugonjwa wa kupooza alionao. Bibi huyo ndiye aliyeficha pesa za Garl na kuzichimbia chini ya ardhi akisema kuwa pesa hizo ni damu ya mjukuu wake MARA iliyomwagika kwaajili ya pesa hizo.

Amante anaamua kutangaza donge nono la shilingi milioni 10 kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa  ya kumpata MARA. Kumbuka kuwa Clara alihamia kwa “Amante” akitegemea kuwa MARA hatokuwepo tena lakini mambo yamekwisha badilika, sasa aamua kufanya uchunguzi wa kuweza kubaini ukweli kama kweli Christian anamficha MARA? Clara anawasili kwao Christian na kumkuta mama yake Christian, wakati mama huyo akimuandalia chakula, mara Clara anaamua kufungua begi la Christian na kukutana na picha alizompiga MARA za hivi karibuni, lakini katika kitendo cha kumaliza kuirudisha camera, Christian anambamba.

Jambazi wa Garl aliyeko jela anampigia simu Garl na kumuuliza kuhusiana na ahadi aliyokuwa amemwahidi kuipatia fedha familia yake ili asitoboe siri kwa polisi, mbona hakuitimiza? Asipofanya hivyo kwa muda mfupi basi atatoboa ukweli, kwani Amante amemwahidi kumpatia milioni 10.

Garl anachukua uamuzi wa kumtuma mwanamke mmoja ambaye alijifanya rafiki ya mke wa jambazi aliyeko jera na kumtuma ammpelekee chakula chenye sumu. Jambazi anafanikiwa kukila chakula kile, ghafla anaanza kutapika kile chakula.

Garl anampigia simu Clara aondoke mara moja pamoja na Alvira katika nyumba yao. Clara anajifanya mgonjwa usiku huo, inabidi Alvira ampeleke hospitali usiku huo. Kumbe Garl anawatuma watu na kuiripua nyumba ya Amante.

Je nini kitaendelea?. Tazama Star TV na karibu tena kwa dondoo  nyingine za tamthilia hii hapa hapa.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.