Header Ads

Breaking News
recent

PAPA MPYA WA KANISA KATOLIKI DUNIANI APATIKANA.

Kiongozi  mkuu wa kanisa Katoliki duniani (Papa) usiku huu kupitia kituo cha matangazo cha BBC maelfu ya waumini wa kanisa Katoliki duniani, wameshudia moshi mweupe kutoka jumba maalum katika kanisa la Sistine Chapel huko Vatican , Roma. ambamo ndimo upigaji kura ulimofanywa na makadinali 115 tokea jana.

Kwa mujibu wa utaratibu wa kanisa Katoliki, wakati wa kumchagua Papa, moshi mweusi huashiria kuwa bado hajapatikana Papa mpya katika uchaguzi huo. Na moshi mweupe huashiria kupatikana kwa Papa mpya atakaeliongoza kanisa  Katoliki duniani kote kama unavyoonekana hapo juu na hapo chini katika video.

Matokeo zaidi ya jina atakalolitumia Papa mpya  atakaeliongoza kanisa Katoliki duniani ikiwa ni baada ya aliyekuwa papa Benedict wa 16 kujiuzulu wazifa wake hivi karibuni, litatambulika mara baada ya kutangazwa rasmi.

TAZAMA PIA  VIDEO HII  KUTOKA "ALJAZEERA"

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.