VIDEO YA MAZIKO YA PADRE 'EVARIST MUSHI' HUKO ZANZIBAR.
Ibada maalum ya kumuombea Padre Evarist Mushi imefanyika leo
Zanzibar kwenye kanisa katoliki la St. Joseph la Minara miwili na kuongozwa na
Askofu mkuu Muadhama Polycarp Cardinal Pengo na kuhudhuriwa na mamia ya waumini
wa kanisa hilo.
Wengine waliohudhuria ni viongozi mbalimbali wa kiserekali
wakiongozwa na Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Ali
Mohamed Shein ambapo baada ya ibada safari ya kuelekea Kitope kwenye maziko
ilianza kwa msafara wa magari mengi kupita mitaani huku ukiongozwa na gari la
Polisi.
Padri Evarist Mushi wa Kanisa katoliki la St Joseph la
Minara Miwili aliuwawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana wakati
akielekea kwenye ibada ya jumapili ya Kanisa la St. Theresia lililoko Mtoni.
Via - millardayo.com
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA