Kiongozi wa dhehebu la la waroma duniani , Papa Benedict wa 16
ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo siku ya jumatatu saa 2 usiku
tarehe 28.2 2013.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 85 amesema
amuamua kujiuzuru katika nafasi hiyo maana hana nguvu tena za kusimamia
shughuli hizo kutokana na uzee pia na matatizo ya kiafya.
Kiongozi huyo ambaye alikuwa ni papa wa 265, alianza kazi zake April
19, 2005 na atakuwa ni papa wa kwanza kujiuzulu kwa karne 6 zilizopita.
Kadinali mkuu wa Vatican atasimamia shughuli zake hadi pale watakapochagua Papa mwingine.
SOURCE: http://goo.gl/ATmbQ
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA