MAMA WA SHARO MILIONEA AFUNGUKA KUHUSU GARI ALILOLIACHA MWANAE.
| Gari aina ya Toyota Opa aliyoiacha marehemu Sharo Milionea. |
Na Gladness Mallya
MAMA wa aliyekuwa msanii wa muziki na filamu Bongo, Hussein
Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’ amefungukia gari aliloacha mwanaye pamoja na
mimba ambayo inadaiwa ni yake.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Mama Sharo alisema:
“Kuhusu gari lile Toyota Opa aliloacha marehemu mwanangu naliuza kwani siwezi
kuliendesha na haliwezi kukaa bila kufanya kazi yoyote.
“Kwa upande wa Marry Lucas wa Sumbawanga msichana
aliyejitokeza baada ya Sharo kufariki na kusema ana ujauzito wake, siwezi
kumtambua kwa sababu enzi za uhai Sharo hakuniambia kuwa ana mchumba wala
mpenzi.”
Sharo Milionea alifariki dunia Nov 26, mwaka jana kwa ajali
ya gari iliyotokea mkoani Tanga.
Siku chache baadaye, Marry aliibuka na kudai alikuwa mpenzi
wa Sharo na ana ujauzito wake.
Source: Global Publishers
Lakini sio vizuri yeye kama mama kumkataa kwa kauli iyo maana vijana wengi hawasemi wakiwa na wapenzi kwa wazazi wao kitu ambacho sio kizuri kwa kweli wengine tujifunze kutokana na makosa,cha mama kufanya angoje azaliwe mtoto kama ni damu ya mwanae asiiache nje angalau akimtazama mjukuu amkumbuke mwanae,inawezekana ni wake au sio wake ila msemakweli ni mtoto.
ReplyDelete