Header Ads

Breaking News
recent

MAMA WA SHARO MILIONEA AFUNGUKA KUHUSU GARI ALILOLIACHA MWANAE.

Gari aina ya Toyota Opa aliyoiacha marehemu Sharo Milionea.

Na Gladness Mallya
MAMA wa aliyekuwa msanii wa muziki na filamu Bongo, Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’ amefungukia gari aliloacha mwanaye pamoja na mimba ambayo inadaiwa ni yake.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Mama Sharo alisema: “Kuhusu gari lile Toyota Opa aliloacha marehemu mwanangu naliuza kwani siwezi kuliendesha na haliwezi kukaa bila kufanya kazi yoyote.
“Kwa upande wa Marry Lucas wa Sumbawanga msichana aliyejitokeza baada ya Sharo kufariki na kusema ana ujauzito wake, siwezi kumtambua kwa sababu enzi za uhai Sharo hakuniambia kuwa ana mchumba wala mpenzi.”
Sharo Milionea alifariki dunia Nov 26, mwaka jana kwa ajali ya gari iliyotokea mkoani Tanga.
Siku chache baadaye, Marry aliibuka na kudai alikuwa mpenzi wa Sharo na ana ujauzito wake.

1 comment:

  1. Lakini sio vizuri yeye kama mama kumkataa kwa kauli iyo maana vijana wengi hawasemi wakiwa na wapenzi kwa wazazi wao kitu ambacho sio kizuri kwa kweli wengine tujifunze kutokana na makosa,cha mama kufanya angoje azaliwe mtoto kama ni damu ya mwanae asiiache nje angalau akimtazama mjukuu amkumbuke mwanae,inawezekana ni wake au sio wake ila msemakweli ni mtoto.

    ReplyDelete

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.