Header Ads

Breaking News
recent

LADY JAY DEE ALIA NA ASKARI POLISI KWA KUTAKA KUMDHALILISHA.

Jana kupitia mtandao wa Twitter mwanadada Lady Jaydee alisimulia kitendo kilimchokera baada ya polisi walioitwa kwenda kumsaidia akiwa kwenye chumba cha hoteli baada ya kuzidiwa ambao waliamua kuwapigia simu waandishi wa habari za udaku waje wapate picha na habari.


“Police mnatumwa kuja kuni rescue mgonjwa Hotel Room, mnaita waandishi waje kuchukua story! Hamjanitendea haki, nimesikitishwa,” alitweet
Jaydee.

“Nawaambia I can’t walk wananilazimisha shuka watu watakubeba gari tumepaki nyuma. Kumbe camera ziko chini huko zinangoja.”

Hata hivyo Jay Dee alivyoulizwa kuwa Waandishi hao walipata walichokitaka Jaydee
alijibu,
“I told them walete doctor humo hotel room kama hawaezi waondoke. Hotel staff told me nsishuke kuna camera chini.”
“Mwenyewe nashangaa hawakuwa wanajali mimi kupata nafuu bali maslahi. Hakuna utu hapo.”
Alimalizia kwa kuandika,
“Hamtujali, na hamjali lolote. Kila mtu ana shida zake ila msichukulie advantage kutunyima haki zetu za msingi. Nimeumia sana!
Hayo ni maneno ya lady Jay Dee

Hata hivyo Jaydeea alidai kuwa kwa sasa anaendelea vizuri ingawa hatukuweza kufahamu alikuwa hoteli gani na wapi pamoja na tatizo lililokuwa likimsumbua ila kwa kile kitakachojiri basi toka kwake tutawajuza.

Stori na Haazu blog.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.