UVUMI WA KIFO CHA MUIGIZAJI MAARUFU 'PETE EDOCHI' ALIYECHEZA FIMAU YA "THINGS FALL APART" WAMALIZIKA.
Mwaka wa 2012 ulikuwa ni mwaka wenye uvumi mwingi wa vifo vya mastaa wa filamu na watu maarufu nchini Nigeria, ambapo miongoni mwa uvumi huo wa vifo ulikuwa ni wa muigizaji mkongwe na maarufu katika fani hiyo kutoka Nollywood - “Pete Edochie”.
Pete amekuwa akicheza uhusika mbali mbali katika filamu toka mwaka 1967 huku akifahamika kwa methali zake na kucheza nafasi ya 'Okonkwo katika movie maarufu ijulikanayo kama "Things Fall Apart" na nyinginezo nyingi alizokwisha zicheza mpaka sasa.
Uvumi uliozuka hivi karibuni kuhusiana na kifo cha muigizaji huyu 'Pete' ni kupitia jina lililokuwa likifanana kidogo na mtu aliyesemekana kufariki - “Hyacinth Peters”lakini wazushi wakageuza maneno na kusema kuwa Muigizaji 'Pete Edochie' alianguka kutoka ghorofani na kufariki kuko nchini Austria mwezi Desemba wakati akitengeneza video ya filamu yake. Lakini uvumi huo umekanushwa na muigizaji mwenyewe "Pete Edochie" mapema mwezi January 4 2013 nyumbani kwake wakati wa mahojiano.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA