SIKU YA MAZISHI YA SAJUKI IKO TAYARI.
Pichani kati ni Naibu Waziri wa Wizara ya
Mawasiliano.Sayansi na Teknolojia,Mh January Makamba akipata maelezo mafupi
kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Filamu
Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba (wa pili kushoto) kuhusiana na mikakati na
mipango mbalimbali ya mazishi ya Marehemu Sadick Juma Kilowoko a.k.a
Sajuki,nyumbani kwao Tabata Bima,jijini Dar.
| Mke wa marehemu Sajuki akifarijiwa na mh. January Makamba. |
Aidha kwa taarifa rasmi kutoka kwa
Simon Mwakifwamba ameeleza kuwa mazishi ya marehemu yatafanyika kwenye makaburi
ya Kisutu siku ya Ijumaa mapema saa tano asubuhi.Kuli kwa Naibu Waziri ni
Mkurugenzi wa utafiti wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba.na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon
Mwakifwamba akitoa maelezo mafupi kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano.Sayansi
na Teknolojia,Mh January Makamba kuhusiana na taratibu mbalimbali kuhusiana na
msiba huo,huku baadhi ya wasanii wengine mahiri wa filamu wakisikiliza kwa
makini.
| Mzee Kilowoko(baba mzazi wa marehemu Sajuki) akifarijiwa |
(PICHA NA IMELDA MTEMA, GPL).. Global Publishers
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA