KIFO CHA SAJUKI ; MSANII WA FILAMU KIMEHUZUNISHA WATANZANIA.
Msanii maarufu wa Filamu nchini Juma Kilowoko(Sajuki)ambaye
hivi karibuni Serikali ilijitolea kubeba jukumu la kugharamia matibabu yake na
hatimaye hivi karibuni kulazwa kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU)
kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili amefariki dunia leo Alfajiri akiwa
amelazwa katika hospitali ya Muhimbili.
Sajuki aalifikishwa hospitalini hapo mwishoni mwa Desemba
2012, alikofikishwa akitokea Amana, alikokuwa akipata matibabu mbaada ya
kuanguka jukwaani jijini Arusha, alipopanda kutaka kusalimia mashabiki wake
ikiwa ni harakati za kutafuta fedha michango ya pesa za kumpeleka tena India
kupata matibabu.
Katibu wa Baraza la Filamu Tanzania (TAFF), Wilson Makubi,
amethibitisha kutokea kwa msiba wa Sajuki, ambaye alikuwa akisubiriwa apate
nafuu ili Serikali ya Tanzania igharamie safari na matibabu yake nchini India.
Makubi alisema kuwa, maandalizi ya msiba huo yatatangazwa
baada ya wahusika na wadau kukukutana, huku akiwataka mashabiki wa sanaa na
msanii huyo kwa ujumla kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha maandalizi ya
mazishio yake.
Kabla na baada ya kuifika India kwa matibabu, Sajuki
aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa uvimbe pembeni ya ini, ambapo aliporejea
alionekana kuimarika kiafya, kabla ya kuanza kuugua tena.
Kifo cha Sajuki kinafanya muendelezo wa vifo vya wasanii
nguli wa filamu na muziki ulioanzia mwaka uliopita, ambapo wakali kama Steven
Kanumba, John Maganga, Mlopelo, Sharo Milionea, Mariam Khamis ‘Paka Mapepe’
walifariki kwa nyakati tofauti kutokana na maradhi na ajali.
Mchakato wa mazishi ya Sajuki unafanyika Tabata, jijini Dar
es Salaam. MUNGU ailaze ROHO ya marehemu SAJUKI mahali pema PEPONI. Ameen
Source: H@ki Ngowi

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA