VITUKO: MARUBANI WAFANYIWA USAHILI KWA KUNUSWA MAKWAPA.
![]() |
Mmojawapo akifanyiwa usahili wa kunuswa kwapa. |
Shirika maarufu la ndege Uchina, limeweka masharti
kwamba mbali na elimu na uzoefu lazima usinuke. Ukiwa mwili wako una harufu
mbaya basi kazi huna. Ni China huko.
Kwa mujibu wa gazeti la SZ News shirika hilo katika kuajiri
marubaNi wapya lazima mtu ananuswa makwapa.
Ukiwa unakikwapa, au makwapa yako yana harufu unanyimwa
kazi.
Kabla ya kuajiriwa katika shirika hilo la ndege. Hatua ya
kwanza ni kunuswa kwapa zako.
Wakuu wa shirika hilo wanajitetea wakisema, kwa vile
marubani wanafanya kazi karibu zaidi na watu basi ni lazima wasiwe na harufu ya
kutisha kwani harufu mbaya ya miili yao au makwapa huenda ikawapunguzia wateja.
Source: BBC
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA