ALICIA KEYS AMTUNUKIA OPRAH WINFREY TUZO YA HESHIMA YA "Keep A Child Alive".
Mwanamuziki wa R&B Alicia Keys amemtunukia tuzo mwanamke mwenye harakati za kijamii duniani mwanamama Oprah Winfrey kupitia mpango wake (Keep a Child Alive) wa kuwasaidia watoto wanaoishi na ugonjwa wa Ukimwi Afrika na India.
Katika sherehe hiyo iliyofanyika jana Alhamis usiku, Alicia Keys aliweza kuchangisha fedha takribani dola milioni 1.3 kwa ajili ya mfuko huo. Milioni moja ilitoka kwa bilionea mmoja aliyefahamika kama Stewart Rahr.
Oprah alianzisha shule ya "Oprah Winfrey Leadership for Girls" mwaka 2007 nchini Africa ya kusini maalum kwa wasichana yatima na wanaishi katika mazingira magumu.
Oprah alimshukuru Alicia Keys kwa kumpatia tuzo ya heshima, kwani alidai kuwa anaamidi kile anachokifanya kinaenda katika njia sahihi ndio maana amefika kupewa tuzo hiyo.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA