WEMA: MAMA USIJE KWANGU HADI..........
Asili Yetu Tanzania.Copyright
![]() |
![]() |
| Wema Sepetu akiwa na mama yake Mariam Sepetu. |
Awali, Wema alieleza kuwa, ameweka utaratibu wa watu kuonana
naye na kwamba wale watakaokwenda kwake bila taarifa watakuwa wanaishia getini.
Maelezo hayo yalimfanya mwandishi wetu amuulize kama hata mama yake akienda kwake bila ‘apointimenti’
hawezi kuingia ndani ambapo alisisitiza kwa kusema kuwa, utaratibu huo ni kwa
watu wote akiwemo mzazi wake huyo.
“Akija bila taarifa hawezi kuingia ndani. Si yeye tu, hata
dada yangu, rafiki yangu yoyote yule, meneja wangu hata wewe kama
sijatoa maagizo kwa walinzi basi ujue utaishia nje na ukinipigia simu huwa
sipokei,” alisema Wema.Kauli hiyo iliwafanya baadhi ya watu kumshangaa kwa
kusema kuwa, utaratibu huo si mzuri kwani kufikia hatua ya kumtaka hadi mama
yake aweke ‘apointimenti’ ndipo amtembelee ni kutafuta laana.
“Huyu anatafuta laana, yaani mama yake asiende kwake hadi
aweke ‘apointimenti’? Yaani kweli mama yake anaweza kufika getini na
asifunguliwe eti kwa kuwa ameenda bila taarifa! Hao wanaomshauri wanampotosha,”
alisema Josephine wa Kinondoni.
Na Shakoor Jongo


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA