WALIOPORA VITU VYA MAREHEMU SHARO MILIONEA WAANZA KUVIRUDISHA KWA SIRI.
![]() |
| Sharo milionea. |
Siku kadhaa baada ya marehemu msanii sharomilionea kuzikwa,
vile vitu ambavyo vilisemekana kupotea ama kuibiwa wakati wa ajali vimeanza
kupatikana.
Akithibitisha habari za kupatikana kwa vitu hiuvyo, swahiba
wake wa karibu ambaye alikuwa akiishi na Sharomilionea Kitale amesema amepata
taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji kule Muheza Tanga kwamba baadhi ya vitu
vimepatikana.
Kwa mujibu wa maelezo yake, vitu ambavyo vilikuwa vimeibwa
ni pamoja nasimu mbili aina ya Blackberry na Samsung, Viatu, Cheni, tairi la
spea ya gari, Betri, Radio ya gari na shilingi milioni sita taslimu ambazo
alikuwa akimpelekea mama yake.
Bwana kitale aliendelea kwa kusema, cha kusikitisha zaidi
katika tukio hilo la wizi, ni unyama uliofanywa na wezi hao ambapo baada ya
kushindwa kumvua pete kwenye kidole cha msanii huyo, waliamua kumkata kidole na
kuondoka na pete hiyo.
Aidha alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa alizonazo kutoka
kwa mwenyekiti wa kijiji kuna wanakijiji wamerudisha baadhi ya vitu kama Simu
ya Mkononi,Pete,Cheni, Jeans, T-shirt,Viatu, ambapo walisema wamerudisha baada
ya kugunduliwa na wanakijiji wenzao ambao walitoa taarifa baada ya kugundua
vitu walivyokuwa navyo ni mali ya marehemu msanii Sharomilionea.
Kitale alisema “kuna kijana mmoja anayeitwa David ambae ni
ndugu na mwenyekiti na wenzake ambao walitajwa na wanakijiji wenzao kwa
kuhusika yeye pamoja na wenzake kufanya kitendo hicho ya bila kujua wanao mfanyia
alikuwa ni Sharro baada ya kutambua watu hao wakafanya ionekane vitu hivyo
vimepatikana kutoka kwa wanakijiji."
Kitale alimalizia kwa kusema kwa sasa vitu ambavyo
havijapatikana ni pamoja na Betri, Tairi la spea, Radio ya gari na pesa ambazo
anasema suala hilo tayari lipo poilisi kwa uchunguzi zaidi.
Hata hivyo habari
zilizotufikia zinadai kuwa Watu wanne
wamekamatwa na Jeshi la Police kwa tuhuma hizo za za kumkata vidole na kumuibia
marehemu Sharo Milionea baada ya kupata ajali ya gari.
Source:Mpekuzi

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA