Header Ads

Breaking News
recent

SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI MKOANI TANGA.

R.I.P SHARO MILIONEA
Habari za kusikitisha zilizotufikia hivi punde, zimeeleza kuwa muigizaji na mchekeshaji mahili hapa Tanzania maarufu kama SHARO MILIONEA amefariki dunia kwa ajali ya gali iliyotokea huko mkoani Tanga leo.
Updates ni kwamba mwendo wa kasi aliokuwa anaendesha marehemu Sharo Milionea ndo ulio sababisha gari kupinduka na kufikwa na mauti. Mama yake mdogo amesema mwili upo hospitali ya Teule wilayani Muheza na kwamba alikuwa peke yake kwenye gari.
 Chanzo Cha Kuaminika: 
Kuhusu kifo cha msanii/mwigizaji Sharo Milionea, namkariri Kamanda wa Polisi Tanga akisema “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”

Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amina.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.