 |
Walter ameandika kwenye profile yake kuwa.....Asante tena ndugu zangu, Nawashukuru ingawa hadi sasa inakuwa ngumu kuamini. Samahani kwa kutojibu sms zenu kama kawaida yangu ni kwa sababu zimekuwa nyingi mnielewe. Nawashukuru sana. ASANTENI SANA tuendelee kuwa pamoja daima.. |
Walter Chilambo alionekana kutawala tukio la jana la kumtafuta star wa Bongo pale Diamond Jubilee ambapo kila alipomaliza kuimba,
MC Vanessa Mdee alisema "hili tamasha limekuwa kama lako!" Walter alifanikiwa kuingia katika round zoote za mchujo na kufnikiwa kunyakua shilingi taslimu milioni 50.
 |
| TOP 5 |
Jamaa kwenye profile yake ya facebook ameandika...."Hadi Ben Pol alinikubali!!
 |
| Salma na Walter wakiwa matumbo joto wakisubili kutajwa mshindi. |
 |
| Hapa ni wakati wakitangaza matokeo ya mshindi wa BSS 2012. |
Hapa Walter akimkumbatia Madam Rita mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi.
Mshidi wa EBSS 2012 Walter Chilambo akikabidhiwa kitita cha milioni 50.
 |
| Umati wa watu ukishuhudia milioni 50 zikikabidhiwa kwa mshindi. |
Na hatimae alimwaga mshiriki mwenzake wa kiume Wababa ambaye watanzania wengi walimpenda akiwa jukwaani lakini walisahau kumpigia kura. Hatahivyo mapambano ya Walter hayakuishia kwa mshiriki mwenzake Wababa bali yalihamia kwa mwanadada mrembo, mwenye mwanya na mtaalamu wa kucheza na gitaa "Salma Yusuf.
 |
| SALMA YUSUF - MSHINDI WA PILI |
Huenda kosa alilofanya Salma, aliimba nyimbo za Kiingereza ambazo hazikuwasisimua wapigaji kura wa Epiq Bongo Star Search ya wakati wa mwisho mwisho, lakini Salma ni mtaalamu, nimkali na hata ukimsikiliza unasahau kama ni mgeni katika game la muziki.
Nafasi hiyo Walter aliituimia kisawa sawa kabisa kwani kutokana na kipaji chake cha muziki wa Bongo flava, alichagua nyimbo zinazopendwa na watanzania wengi. Wimbo wa Ben Pol ndio uliomtajirisha Walter na kumfanya star.... Ben Pol alikili kutendewa haki na msanii Walter pale alipokuwa akiimba wimbo wake kwa mara ya mwisho.... hivyo Ben Pol aliinuka kwenyekiti na kumtunza manoti ya fedha Walter.
 |
| TOP 5 |
VOCALIST - NSAMI NKWABI.... AMEFUNGUKA KUWA...
"Napenda
sana kumshukuru Mungu kwa hatua niliyofikia, napenda pia kushukuru
familia yangu na nyinyi mashabiki wangu kwa kunipenda, kunipa nguvu na
kunishauri nawapenda sana na samahani kwa kuwaangusha wapendwa sauti
iliniharibia mwishoni lakini tupo pamoja sana. Nawapenda sana wapendwa
mbarikiwe na wale wasabato wenzangu sabato njema!"
 |
| Madam Rita na Master J |
 |
| NSHOMA |
 |
| MC'S WA EPIQ BONGO STAR SEARCH 2012. |
 |
| Hii ndio sehemu ya VIP ya shindano la Bongo star Search lilipofanyika pale Diamond Jubilee. |
Washiriki wote walioingia top five, walikuwa ni wakali... so hongereni sana kwa kazi nzuri mliyoionyesha kwa wakati wote mliokuwa mkitizamwa na watanzania wenzenu, sehemu mbali mbali za dunia.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA