Meneja wa Club ya Chelsea Robert Di Matteo amefukuzwa kazi.
Roberto Di Matteo
amefutwa kazi na klabu ya Chelsea, baada ya kuwa meneja kwa kipindi cha miezi
minane.
Di Matteo aliiwezesha Chelsea kuwa mshindi wa klabu bingwa
barani Ulaya, na vile vile kupata Kombe la FA msimu uliopita, na mwezi Juni,
alitia saini mkataba wa miaka miwli.
Lakini kufuatia Chelsea kuzabwa magoli 3-0 na Juventus usiku
wa Jumanne, inaelekea timu hiyo itakuwa na kibarua kigumu sana cha kufanikiwa
kuendelea katika michuano ya klabu bingwa, na kwa hiyo wasimamizi wa klabu
wameonelea ni vyema kumtimua kutoka Stamford Bridge.
Kulingana na taarifa katika mtandao wa Chelsea, "klabu
kitatoa taarifa kamili hivi karibuni kuhusiana na meneja wa timu".
Roman Abramovich, tajiri anayemiliki klabu ya Chelsea, sasa
atakuwa anamtafuta meneja wa tisa, tangu kumiliki klabu mwaka 2003, na kwa muda
mrefu, inaaminika amekuwa akizitamani sana huduma za aliyekuwa meneja wa
Barcelona ya Uhispania, Pep Guardiola.
Lakini vile vile amewasiliana na aliyekuwa kocha wa
Liverpool ya Uingereza, Rafael Benitez, na kuna uwezekano huenda akashikilia
hatamu kwa muda mfupi.
Abramovich, raia wa Urusi, tayari alikuwa amewasiliana na
Benitez hata kabla ya Chelsea kushindwa nchini Italia.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA