SHINDANO LA MFALME WA 'KURAP' KUANZA JUMAPILI HII PALE DAR LIVE.
Asili Yetu Tanzania.Copyright
![]() |
| Picha wakati wa mkutano huo |
SHINDANO kubwa la kumtafuta Mfalme wa Kurap Bongo
lililoandaliwa na Ukumbi wa Dar Live, litaanza Jumapili hii katika ukumbi huo
ulioko Mbagala, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya The
Atriums iliyopo Sinza Afrika jana jijini Dar, Meneja Mkuu wa kampuni ya Global
Publishers Ltd ambao ndiyo wamiliki wa ukumbi huo, Abdallah Mrisho, amesema
mshindi atazawadiwa gari la kifahari ambalo litatangazwa hivi karibuni.
“Kuanzia kesho, vijana wajitokeze pale Dar Live kwa wingi
ili kushiriki. Jumapili ya wiki hii
ndiyo watapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao, na mchakato mzima wa kumtafuta
mshindi ndiyo utakuwa umeanza rasmi,” alisema Abdallah.
Aidha, mratibu wa shindano hilo, Luqman Maloto, amesema watu
wajitokeze kwa wingi kwani hakuna ‘longolongo’ na majaji watakuwa ni watu wenye
heshima kubwa kwenye gemu ya muziki Bongo pamoja na wananchi watakaokuwa
wakihudhuria Dar Live.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA