MTANGAZAJI WA TIMES RADIO "DIDA" ALIA NA USHURU, AINGIZE RANGE ROVER KUTOKA MAREKANI.
Asili Yetu Tanzania.Copyright
HADIJA Shaibu ‘Dida’ ni mtangazaji the big name Bongo
anaye-host program ya Mitikisiko ya Pwani kunako kituo namba moja cha Radio
Times FM cha jijini Dar, ambaye amelia na serikali impunguzie ushuru ili
aingize nchini gari la bei mbaya aina ya Range Rover kutoka pande za Marekani.
Hot 2 Hot kupitia blog ya presenta huyo imeinyaka kuwa
bidada huyo anatamani kuingiza mkoko huo Bongo lakini hofu yake ni juu ya
ushuru unaotozwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) bandarini, hivyo kuomba kupunguziwa
ili naye asukume ndinga hiyo ya bei chafu mjini.
“Jamani TRA nipunguzieni ushuru,” aliandika Dida kwenye
mtandao huo wakati amepozi na gari hilo hivi karibuni akiwa likizo huko New
York, Marekani.
Dida anatarajiwa kushuka nchini mahususi kwa kuongoza shoo
kubwa ya Mitikisiko ya Pwani itakayozikutanisha bendi zote za Taarab
zinazotamba Bongo ndani ya kiwanja cha maraha cha Dar Live, Mbagala-Zakhem,
Novemba 3, mwaka huu.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA