Header Ads

Breaking News
recent

MAJAJI WA EPIq BONGO STAR SEARCH WASHINDANA VIKALI.

Asili Yetu Tanzania.Copyright

Majaji wa BSS 'Madam Rita na Master J' wakionyesha kuchuana vikali jana jumapili katika BSS.
Hii ndio timu ya Madam Rita - Wababa Mtuka, Nshoma na Walter Chilambo.
Timu ya Master J - Salma Yusuf, Norman Severino na Godfrey Levis.
Timu ya Salama Jabir - Husna Kidoti, Nsami Nkwabi na Mwenyna Atiki.
MCHUANO mkali ambao huwa kati ya washiriki wa Epiq BSS, jana ulibadilika na kuwa baina ya majaji, ambao kwa wiki hii kila jaji alipewa washiriki wa kuwanoa kwa wiki nzima ili waje waoneshe uwezo wao.

Washiriki wote kuanzia walionolewa na Master J, Salama Jabir na Ritha Paulsen, walionekana kufanya vema huku wale waliofundishwa na Master J, walionekana kufunika zaidi.

Mshiriki wa kwanza kuanza kuimba alikuwa ni Godfrey Kato aliyeimba wimbo wa Ommy Dimpozi wa baadaye, Salma aliimba wimbo wa Papa Wemba wa Rain On huku Norman Severino akiimba wimbo wa Kidumu, Nitafanya.

Mbali ya kuonesha uwezo wa kuimba, pia waling’ara kwenye utundu wa kuweka vionjo vyao katika nyimbo hizo hali iliyoamsha shangwe kwa majaji hasa washiriki wao walipopanda jukwaani.

Kilichovutia zaidi katika kipindi cha jana ni kitendo cha majaji kukosoana uwezo wao wenyewe wa kuwaandaa washiriki, huku kila mmoja akijisifia kuwa ameweza kuandaa washiriki wake.

Kwa upande wake Jaji Mkuu, Madam Ritha, alikuwa na washiriki kama vile Nshoma aliyeimba wimbo wa ‘Hapo Zamani’ wa Miriam Makeba, Wababa aliimba wimbo wa ‘Valuvalu’ wa Chameleon huku Water Chilambo akiimba wimbo wa ‘Mawazo’ wa Diamond.

Katika kundi hili wote waliimba vema lakini mshiriki Wababa alionekana kufunika zaidi kwa kuwa alishangiliwa kuliko washiriki wote wa jana huku Nshoma akionekana kuwa alipendeza zaidi kwa vazi alilovaa lililoendana na wimbo wake.

Jaji Salama alikuwa na washiriki Husna aliyeimba wimbo wa ‘Kidudu Mtu’ wa kundi la Offside Trick, Menynah aliyeimba wimbo wa Nyota Ndogo uitwao ‘Watu na Viatu’ huku Nsami akiimba wimbo wa Lady Jaydee wa ‘Nilishakuaga na Wangu’.

Katika kundi hili Husna alionekana kumbeba zaidi Salama kwa kuwa aliimba na kucheza vema kimvuto zaidi na kupigiwa kelele nyingi za kushangiliwa lakini hata wengine nao waliimba vema.

Wakati shindano linakaribia fainali, ambayo itafanyika mwezi ujao, mashabiki wanaombwa waendelee kuwapigia kura washiriki wanaowapenda ili waweze kufika fainali.

Washiriki waliobaki na namba zao za ushiriki: EBSS 01, Godfrey Kato; EBSSO2, Husna Nassor; EBSSO4, Menynah Atiki; EBSSO5, Norman Severino; EBSS06, Nsami Nkwabi; EBSS07, Nshoma Ng’hangasamala; EBSS09, Salma Abushiri; EBSS10, Vicent Mushi; EBSS11, Wababa Mtuka; na EBSS12, Walter Chilambo.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.