ASILI YETU BLOG: MISS EAST AFRIKA 2012.
Asili Yetu © All rights reserved
Mrembo atakaeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya mwaka
huu ya urembo ya Miss East Africa atatangazwa rasmi tarehe 14/10/2012 katika
hotel ya Serena Jijini Dar es salaam.
Jumla ya warembo 148 wameomba kuiwakilisha Tanzania katika
mashindano ya Miss East Africa mwaka huu lakini ni Mrembo mmoja tu
atakaechaguliwa kuiwakilisha Nchi katika mashindano hayo makubwa ya urembo
katika ukanda huu wa Africa na yanayosubiliwa kwa hamu na wapenzi wa fani hiyo
ndani na Nje ya Africa Mashariki.
Aidha maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri
ambapo yatafanyika tarehe 07 December, 2012 katika ukumbi wa Mlimani City
Jijini Dar es salaam.
Wakati huohuo Nchi ya Burundi imebadili mwakilishi wake
ambapo sasa itawakilishwa na mrembo Ariella Kaneza (23), Mwanafunzi wa mwaka wa
pili wa chuo kikuu cha Universte De Lumiere akichukua Degree ya marketing.
Taarifa kutoka Burundi iliyosainiwa na Mratibu wa Mashindano
ya Miss East Africa Nchini humo, Serge Nkurunziza, zimeeleza kwamba Burundi
imeamua kubadili mwakilishi wake ili kuhakikisha kwamba Nchi hiyo inashinda
Taji hilo kwa mara ya pili tangu mashindano hayo yalipoanzishwa mwaka 1996
baada ya kugundua kwamba mwakilishi wake wa awali anapungukiwa baadhi ya sifa
chache za kuweza kunyakua taji hilo. (Burundi imewahi kushinda Taji hilo mara
moja mwaka 2008 kupitia kwa mrembo wake Miss Claudia Niyonzima.
Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu yanatarajiwa kuwa
na mvuto wa aina yake na yatashirikisha warembo kutoka Nchi 16 za ukanda wa
Afrika Mashariki.
Nchi zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni wenyeji
Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine zilizoalikwa kushiriki
ni pamoja na Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Southern Sudan, Malawi,
pamoja na visiwa vya Seychelles, Madagascar, Reunion, Comoros, na Mauritius.
Mashindano ya Miss East Africa yanalenga kukuza ushirikiano
na kutangaza utamaduni wa Afrika Mashariki, pamoja na kutangaza utalii wa
Tanzania kama Nchi wenyeji wa mashindano hayo makubwa katika ukanda huu wa
Afrika.
Mashindano ya Miss East Africa yanamilikiwa na kuandaliwa na
kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam,.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA