Header Ads

Breaking News
recent

"YU WENXIA" MREMBO KUTOKA CHINA ACHUKUA UREMBO WA DUNIA 2012

Asili Yetu © All rights reserved

                                            Mrembo wa dunia 2012 "Yu Wenxia" kutoka China.

 Mashindano ya urembo wa dunia yaliyolindima leo jumapili katika jiji lenye  migodi ya madini la Ordos katika viunga vya jangwa la Gobi - Mongolia - Beijing China, limemalizika baada ya miss China "Yu Wenxia" kuwatupia vumbi takribani warembo 100 kutoka katika pembe za dunia kawa kuchukua tuzo hiyo ya urembo wa dunia.

 Yu Wenxia (kati kati) kutoka China amenyakua tuzo ya mrembo wa dunia 2012 huku nafasi ya pili akichukua mrembo Wales Sophie Woulds (kushoto) na nafasi ya tatu ilinyakuliwa na miss Australia Jessica Kahawaty.

Mashindano ya kumsaka mrembo wa dunia, ni kati ya mashindano yaliyoanza kitambo huko nchini Uingereza mwaka 1951. Mwanzirishi wa mashindano hayo alifahamika kama "Eric Morley". Kwa kawaida wakati ule washiriki wa urembo walikuwa wakitangazwa katika sherehe maalum za waingereza na baada ya hapo ulikuwa ni utamaduni wao kuwa mshindi anakuwa  ndiye mrembo wa mwaka huo mzima jijini London na anapata nafasi ya kusafiri duniani akiliwakirisha shirika la urembo duniania (MWO).

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.